Friday, April 18, 2014

Dk. Salim kushuhudia Usiku wa Mwambao Asilia Jumamosi hii April 19

“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan, ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asilia za zamani na za sasa.”
..............
 
Na Andrew Chale
 
KATIBU Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa ya Afrika (OAU, sasa Umoja wa Afrika - AU), Dk. Salim Ahmed Salim, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onesho maalum la Usiku wa Mwambao asilia utakaosindikizwa na bendi za  Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii April 19
 
Mlezi wa heshima wa kundi la Dar Modern Taarab, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, alisema Dk. Salim ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, amethibitisha kujumuika na wadau na mashabiki wa taarabu asilia.
Idarous alisema wadau wa muziki wa taarabu watafurahia usiku huo wa Mwambao Asilia kutoka kwa wanamuziki nguli wa miondoko hiyo Bara na Visiwani.

“Usiku wa Mwambao Asilia, utasheheni magwiji wakongwe wa muziki wa taarabu nchini, kutoka kundi la Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan, ambao wataporomosha nyimbo za taarabu asili za zamani na za sasa,” alisema Idarous.

Aliongeza kuwa pia usiku huo utapambwa na ‘surprise’, ikiwemo watu mbalimbali kupita kwenye zulia jekundu ‘red carpet’ na kupiga picha za ukumbusho na mastaa watakaohudhuria.
Alisema katika usiku huo, kiingilio kitakuwa ni sh 10,000 ambapo tayari tiketi zilishaanza kuuzwa sehemu mbalimbali.

Idarous alizitaja sehemu hizo kuwa ni duka la Fabak Fashions, Regency Park Hotel Mikocheni na Dar Modern Taarab Hall Magomeni Ifunda.
Onyesho hilo pia limedhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com

Mzee Mwinyi atembelea banda la Mamlaka ya usafiri wa Anga katika Maadhinisho ya miaka 50 ya uhuru

Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

DKT. BILAL AWASILI MJINI UNGUJA KUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO KESHO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Wa pili (kulia) ni mkewe Mama Zakia Bilal. 
Picha na OMR

KUTOKA KWA MTUME NA NABII TB JOSHUA:Supernatural Healing | Sleep Apnea | TB Joshua

NEWS ALERT: MELI YA MIZIGO YAZAMA ZIWA VICTORIA

Meli ya mizigo ya Kampuni ya FB Matara iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza ikiwa na wafanyakazi 10 na shehena ya sukari imezama Ziwa Victoria katikati ya visiwa vya Kerebe na Bumbile 

Tutawajuza kadri taarifa zinavyotufikia kutoka kwa mdau wetu 

TANZANIA NI NCHI YA AMANI

MAGARI MAWILI YAGONGANA MAFIATI MKOANI MBEYA MUDA MFUPI ULIOPITA

Wakazi wa eneo la Mafiati Mkoani Mbeya wakishuhudia ajali iliyotokea katika eno hilo muda mfupi uliopita na kuhusisha magari madogo mawili moja likiwa ni Mazda yenye namba za usajili T935 BJP na gari nyingine Toyota Gaia ambayo namba zake hazikupatikana kwa haraka
Gari yenye namba za usajili T 935 BJP ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya kugongana na gari nyingine ndogo aina ya Toyota Gaia (haipo pichani) katika eneo la Mafiati Mkoani Mbeya. Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Wakazi wa Mafiati Mbeya wakilitazama gari aina ya Mazda yenye namba za usajili T935 BJP jinsi ilivyoharibika mara baada ya kupata ajali kwa kugongana na gari ndogo aina ya Toyota Gaia muda mfupi uliopita katika Eneo la Mafiati Mkoani Mbeya, Nyuma ni gari aina ya Toyota gaia iliyogongana na Gari hiyo aina ya Mazda.
 Wakazi wa Mafiati wakilitazama Gari aina ya Toyota Gaia ambazo namba zake hazikuweza kupatika kwa haraka mara baada ya kugongana na gari aina ya Mazda katika Eneo la Mafiati Mkoani Mbeya muda mfupi uliopita.
 Gari aina ya Toyota Gaia ikiwa imeharibika pembeni kama inavyoonekana katika picha. Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog - Mbeya

The youths fight for 100/-

THE youths above fight for 100/-, which one of them (right) collected from a pedestrian who had used the stones they had arranged to step on and avoid wading in sewerage along Msimbazi Street in Dar es Salaam. (Photo by Robert Okanda)

Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba, Azuia Benki kuwalipa "UKAWA" waliokimbia Bungeni

Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba, Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.


Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.

Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.

Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu  kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile. 

Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.

Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MBEYA ZAMU YENU SASA IMEFIKA