AFISA UHUSIANO TTCL AFARIKI DUNIA | LUKAZA BLOG

AFISA UHUSIANO TTCL AFARIKI DUNIA

  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga. OFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),...

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga. 
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga.

OFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga, amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016.

Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi.

"...Ni kweli, Bi Amanda amefikwa na umauti akiwa likizoni mkoani Mbeya alikokwenda kuwasalimu ndugu zake.. Aliugua ghafla Alhamisi hii na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo Mungu alimchukua," alisema Bw. Thom Mushi.

Alifafanua kuwa mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya kwenda Njombe na Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar 29.02.2016 katika Kijiji cha Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe.

Mtandao huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi. Amanda Fredrick Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.

Related

Kijamii 381911598157965228

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item