Fahamu aina tano za mitungi ya kuzimia moto | LUKAZA BLOG

Fahamu aina tano za mitungi ya kuzimia moto

1.MTUNGI WA MAJI(WATER) Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingin...


1.MTUNGI WA MAJI(WATER)

Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana kuutumia kwenye moto wa umeme

2. MTUNGI WA KABONDAYOKSAIDI(CO2)

Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya baridi sana unaweza kuganda.

3. MTUNGI WA POVU(FOAM)

Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na vitu vigumu

4. MTUNGI WA PODA(POWDER)

Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.

5. MTUNGI WA DAWA/KEMIKALI(Chemical)

Mtungi huu una lebo ya NJANO kama kitambulisho chake. Unazima aina nyingi za moto ukiwamo wa mafuta.

KUMBUKA: Mtungi wa kuzimia moto si kwaajili ya kuufanya moto usiendelee kuwaka bali kukufanya upate njia ya kujiokole hasa ukiwa ndani ya nyumba yako. Kwa udogo wa ule mtungi huwezi kuzima moto
unaunguza nyumba nzima. Kama moto umezuia mlango, chukua mtungi elekeza pale
mlangoni ili moto uzimike upate kwa kutokea Unapozima elekeza bomba la tingisha chini ulipo mot sio juu ya moto.Imeandaliwa na RSA na Dj sek Blog

Mitungi ya zimamoto hutofautishwa kutokana na lebo za rangi zake (codes). Mfano Dry powder-Bluu; Kabondayoksaidi-Nyeusi. Na kila mmoja una kazi maalumu tofauti na mwingine. Penginepo hutumia herufi A,B,C
Herufi A ni kwa mtungi unaozima moto wa karatasi,mbao, plastiki,nguo,mipira na takataka
Herufi B ni kwa mtungi unaozima moto wa gesi,mafuta, rangi na solventi
Herufi C ni kwa mtungi unaozima moto wa nishati kama umeme na mafuta.  Kwa kupata Mitungi au huduma ya Vifaa vya Zima Moto Basi tembelea ofisi za Catranic Zilizopo Mtaa Ursino Mikocheni

Related

Makala 3251096509297535231

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item