Producer wa filamu ya Mpango Mbaya Staford Kihole Kutua Nchini Nigeria | LUKAZA BLOG

Producer wa filamu ya Mpango Mbaya Staford Kihole Kutua Nchini Nigeria

MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu ambaye pia ni mwasisi wa Mtandao huu FC Staford Kihore anatarajia kutua nchini Nigeria kwa ajili y...

MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu ambaye pia ni mwasisi wa Mtandao huu FC Staford Kihore anatarajia kutua nchini Nigeria kwa ajili ya kushuhudia utoaji wa tuzo za African Magic Views Choice Awards tuzo hizo ambazo zinatarajia kutolewa mwezi March 2016, akiongea na FC Kihore amesema kuwa anatarajia kutua Lagos tarehe 2 March. 2016.

Mtayarishaji huyo ambaye pia ni muongozaji wa Tmt anakwenda kama mmoja wa watayarishaji wanaogombea tuzo huku yeye akipelekwa na filamu ya Mpango mbaya kazi bora kazi kutoka Swahilihood ikishirikisha wasanii nyota waliopikwa kutoka katika mradi mkubwa kabisa wa Tanzania Movie Talent (TMT).

“Nitakuwepo kwa siku kadhaa nchini Nigeria kwa matukio makuu mawili au hata matatu kwanza kabisa ni kushudia utoaji wa tuzo nikishiriki kupitia filamu ya Mpango Mbaya, jambo la pili ni kuonana na kubadilishana mawazo na watengeneza filamu wakubwa kutoka sehemu mbalimbali za Afrika,”anasema Kihore.

Unapomuongelea Staford Kihore ana sifa ya kipekee kwani ndio Producer pekee aliyeweza kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu bila yeye kuwa mwigizaji kama historia ya watayarishaji wengi wa Swahilihood ambao wengi ni waigizaji mtayarishaji huyu amekuwa ndio mtayarishaji wa kwanza kutengeneza filamu za bajeti kubwa.

Na unapoongelea miradi mingi sana ya tasnia ya filamu Swahilihood hususani project za Filamucentral anahusika sana kama tuzo za BORA 2010, DAR FILAMU FESTIVAL (DFF 2013) ni mratibu na mwasisi pia sisi menejimenti ya FC tunajivuania mtu muhimu sana kwa maendeleo ya tasnia ya filamu Bongo.

Mwaka 2010 aliweza kutengenza filamu ya CPU kazi ambayo iliamsha ari kwa baadhi ya watengnezaji wa sinema kujiamini na kuanza kufuata nyayo zake kwani sinema hiyo iliweza kuonyeshwa katika majumba ya sinema na kushangiliwa sana na watazamaji, kila mara ukiongea Staford ni mtu anayependa mapinduzi katika tasnia ya filamu.

“Naweza kusema tasnia inapiga hatua na kila sehemu nayokwenda kwa safari za kikazi nafanya utafiti utakaoleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu na kuwa Industry kubwa Afika kila mtu awajibike alipo,”Kihore.

Ni matarajio yetu sisi kama wadau wakubwa wa tasnia ya filamu Swahilihood kuwa Kihore anapokkwenda Nigeria anarudi na ushindi mkubwa sambamba na tuzo FC inamtakia kila heri katika kupigania tasnia ya filamu Swahilihood.

Related

Filamu 8321775963033015604

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item