Tazama hapa magoli ya yaliyofungwa na Messi katika Mchezo wa UCL kati ya Barcelona na Arsenal jana | LUKAZA BLOG

Tazama hapa magoli ya yaliyofungwa na Messi katika Mchezo wa UCL kati ya Barcelona na Arsenal jana

Image copyright PA Image caption Barcelona yaiadhibu Arsenal kwa mabao 2-0 Klabu ya soka ya Barcelona imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa...

Image copyrightPA
Image captionBarcelona yaiadhibu Arsenal kwa mabao 2-0
Klabu ya soka ya Barcelona imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA) mchezo uliopigwa uwanja wa Emirates. Mabao ya Barcelona katika mchezo huo yamefungwa na mchezaji Lionel Messi dakika ya 71 na Dakika ya 83 likiwa ni bao la pili lililofungwa kwa njia ya penati .
MessiImage copyrightAP
Image captionMessi alifunga mabao yote mawili
Katika mchezo mwingine Juventus wakiwa nyumbani dhidi ya Buyern Munich, mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2.
Bayern Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen Robben akaandika bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha pili.
Kwa upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.
Michuano hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man City huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi dhidi ya Atletico Madrid.Chanzo BBC Swahili

Related

Michezo 7461380685880148214

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item