KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA BOHARI YA DAWA MSD JIJINI DAR ES SALAAM LEO | LUKAZA BLOG

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA BOHARI YA DAWA MSD JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD...

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Banakunu (kulia), wakitembea wakati kamati hiyo ilipotembelea MSD Makao Makuu Keko Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Mary Lingo (wa pili kulia), akiwaelekeza wajumbe wa kamati hiyo jinsi dawa zinavyotunzwa katika maghala.
 Mkurugenzi wa MSD, Laurean Banakunu (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea MSD leo.
Mjumbe wa kamati hiyo, Azani Zungu akiuliza swali juu ya kuharibika kwa dawa.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Jamii imetembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa Keko na kuipongeza kwa utendaji wake kazi pamoja na mazingira magumu yanayoikabili.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba amesema Kamati yake itasimamiana kuyafanyia kazi masuala makubwa manne ambayo ni pamoja na bajeti finyu ya dawa, ulipwaji wa deni la serikali, mfumo wa uwajibikaji kati ya Tamisemi na Wizara ya Afya ambao unasababisha utekelezaji na usimamizi wa masuala ya Afya kutokuwa na mtiririko kutoka juu kwenda chini. 

Jambo la nne ni kuhakikisha utekelezaji wa kuongeza uzalishaji dawa ndani ya nchi kupitia sekta binafsi (PPP).

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangala alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Bohari ya Dawa inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kwa bei nafuu, hivyo Serikali imeweka kipaumbele kuhakikisha deni la MSD linalipwa mapema iwezekanavyo.

Alisema tayari Wizara ya Afya imeiagiza MSD kuandaa bei elekezi kwa maduka maalum ya dawa (prime vendor) ili vituo vinavyokosa dawa MSD vinunue huko bila usumbufu na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa dawa na vifaa tiba.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameviomba vituo vya Afya kuleta mahitaji yao kwa wakati.

Related

kitaifa 8763978524981328895

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item