Kigoma kunufaika na vipimo vya ugonjwa wa Moyo kutoka kwa Daktari Bingwa Masatu | LUKAZA BLOG

Kigoma kunufaika na vipimo vya ugonjwa wa Moyo kutoka kwa Daktari Bingwa Masatu

  DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said WATU wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mk...

 DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WATU wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa mapema Aprili 4 hadi 9, 2016,  kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt. Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema, huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na ECHO  zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.
Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.


 Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo

Related

Hot Stories 1804483164119995659

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item