Leicester City kukutana na Barcelona | LUKAZA BLOG

Leicester City kukutana na Barcelona

Leicester wameshangaza wengi msimu kwa kukwamilia kileleni Klabu ya Leicester City ya Uingereza itacheza dhidi ya miamba...

Leicester
Leicester wameshangaza wengi msimu kwa kukwamilia kileleni

Klabu ya Leicester City ya Uingereza itacheza dhidi ya miamba wa Ulaya, klabu ya Barcelona kutoka Uhispania, Agosti mwaka huu.
Klabu hizo zitakutana katika dimba la Kombe la Mabingwa wa Kimataifa ambalo huchezwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Viongozi hao wa Ligi ya Uingereza pia watakutana na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain.
Leicester watakutana na Celtic mjini Glasgow tarehe 23 Julai, PSG mjini Los Angeles tarehe 30 Julai na Barcelona mjini Stockholm tarehe 3 Agosti.
Barcelona ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya

Klabu hiyo ni miongoni mwa klabu tano za Ligi ya Uingereza zitakazoshiriki michuano hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa huchezewa Marekani.
Klabu nyingine kutoka Uingereza ni Manchester United, Liverpool, Manchester City na Tottenham Hotspur.
Msimu mpya wa Ligi ya Premia utaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti.
Ratiba ya Mechi za Klabu Bingwa Kimataifa
 • 23 Julai - Celtic v Leicester, Glasgow
 • 24 Julai - Inter v PSG, Eugene
 • 27 Julai - Real Madrid v PSG, Columbus
 • 27 Julai - Bayern Munich v AC Milan, Chicago
 • 27 Julai - Chelsea v Liverpool, Pasadena
 • 30 Julai - Celtic v Barcelona, Dublin
 • 30 Julai - Inter v Bayern Munich, Charlotte
 • 30 Julai - AC Milan v Liverpool, Santa Clara
 • 30 Julai - PSG v Leicester, LA
 • 3 Agosti - Barcelona v Leicester, Stockholm
 • 3 Agosti - Bayern Munich v Real Madrid, East Rutherford
 • 3 Agosti - AC Milan v Chelsea, Minnapolis
 • (Kuthibitishwa baadaye) - Liverpool v Barcelona
 • (Kuthibitishwa baadaye) - Inter v Celtic
 • (Kuthibitishwa baadaye) - Real Madrid v Chelsea

Related

Michezo 7475262798531290475

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item