WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI PAMOJA NA WAFANYABISHARA WADOGO WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA MAONYESH YA MADINI MERERANI | LUKAZA BLOG

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI PAMOJA NA WAFANYABISHARA WADOGO WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA MAONYESH YA MADINI MERERANI

  kamishina wa madini kanda ya kaskazini Elius Kayandabila akiwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya maandalizi ya maony...

 kamishina wa madini kanda ya kaskazini Elius Kayandabila akiwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya maandalizi ya maonyesho ya madini na vito yanayotarajiwa kuanza hapo kesho ndani ya mji mdogo wa mererani

Na Woinde Shizza,Arusha

Wachimbaji wa madini ya vito nchini wametakiwa kushiriki katika maonyesho ya wachimbaji wadogo wa madini ili kuweza kutumia fursa hiyo ya kuuza na kupanua wigo wa kupata masoko ya ndani na nje ili kuweza kukuza uchumi wao na pato la taaifa.

Hayo yameelezwa leo na kamishina wa madini kanda ya kaskazini Elius Kayandabila wakati akiongea na waandishi wa habari  kuhusiana na maandalizi ya maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza kesho march 9 hadi kumi katika mji mdogo wa mererani uliopo mkoani Manyara.

Hata hivyo amesema kuwa lengo haswa ni kuonyesha madini hayo ya wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo kuwakutanisha na wafanyabiashara wakubwa wa ndani ya nchi ambapo maonyesho hayo yatawasaidia pia kupata masoko kwa urasi

Aidha ameongeza kuwa wachimbaji zaidi ya 50 watashiriki maonyesho hayo ya madini katika mji mdogo wa marerani ambapo hii ni kwa mara ya kwanza maonyesho hayo kufanyika eneo hilo ,ambapo alifafanua kuwa maonyesho haya pia ni moja ya maandalizi ya maonyesho makubwa ya kimataifa ya vito na madini  ambayo hufanyika kila mwaka mjini Arusha .

Kayanda bila aliwataka wachimbaji hao kuweza kutumia fursa hiyo ya maonyesho haya ili kuweza kujifunza na kupata masoko ya ndani na nje kwa uhakika huku akiwasihi wakazi wa jiji la arusha pamoja na mkoa wa manyara kujitokeza kwa wingi kuangalia aina mbalimbali za madini zinazopatikana hapa nchini.

Aidha pia alitumia fursa hiyo kuwasihi wafanya biashara wadogo na wakubwa ambao wanafanya biashara ya madini kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya ili kuweza kupata madini hayo kwa bei nafuu na kuweza kufaamiana zaidi na wachimbaji wadogo pamoja na wafanyabiashara wadogo wa madini.

Related

kitaifa 7827532190180481260

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item