Bilionea Al Fahim awa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon | LUKAZA BLOG

Bilionea Al Fahim awa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon

Mfanyabiashara maarufu wa kiarabu Dk Sulaiman Al-Fahim ametangazwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon ambayo itashiriki li...

Mfanyabiashara maarufu wa kiarabu Dk Sulaiman Al-Fahim ametangazwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon ambayo itashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.


Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi alisema kuwa waliamua kumuomba Al Fahim kushika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake katika michezo hasa mpira wa miguu mbali ya kuwa mfanyabiashara bilionea katika nchi za Uarabuni na duniani kwa ujumla.

Kangezi alisema kuwa Al Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate Development ya Dubai na miaka ya nyuma alikuwa msemaji wa kampuni inayomiliki klabu tajiri duniani, Manchester City, Abu Dhabi United Group (ADUG).

ADUG ilinunua Manchester City mwaka Septemba, 2008.

Pia Al Fahim alitaka kununua klabu ya Portsmouth ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu ya Uingereza, lakini mpango huo haukuweza kukamilika.

Kangezi alisema kuwa Al Fahim ataanza kazi rasmi Aprili 16 ambapo atatangaza timu yake ambayo atafanya nayo kazi katika kuibadili klabu hiyo na kuwa klabu bora Tanzania na Bara la Afrika.

Alisema kuwa uwepo wa Al Fahim kuitaifanya timu hiyo kuwa na uongozi bora wenye kujua uendeshaji wa kisasa katika masuala ya mpira kwa kuzingatia uzoefu wa mfanya biashara huyo mzoefu katika soka na michezo mengine.

“Haikuwa kazi rahisi  Al Fahim kukubali kuingia kwenye uongozi wa klabu yetu, ila tunashukuru kwani alituelewa baada ya kukutana naye alipokuja hapa nchini kwa shughuli zake, “ alisema Kangezi.

Alisema kuwa lengo lake ni kuona African Lyon inakuwa klabu ya mfano sit u kwa Tanzania, hata kwa nchi za Afrika Mashariki na  Afrika kwa ujumla. Kangezi alisema kuwa mipango yao ya awali ni kuhimarisha timu ya kwanza ili  iweze kufanya vyema katika mashindano ya ligi kuu na pia kuanzisha msingi mzuri wa timu za watoto.

 “Dk Sulaiman ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Al Fahim Group na vile vile alikuwa mkurugenzi wa kituo cha Royal Football Fund (RFF) mbali ya kuwa mchezaji wa mchezo wa chesi, ameahidi kusaidia wachezaji chipukizi ili kuwawezesha kushiriki katika mpira wa kulipwa, tunaamini titafika, ” alisema.

Related

Michezo 3682281584411786235

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item