Bomoa Bomoa Jimbo la Segerea kuendelea, Mahakama Kuu yatupilia mbali kesi | LUKAZA BLOG

Bomoa Bomoa Jimbo la Segerea kuendelea, Mahakama Kuu yatupilia mbali kesi

Baadhi ya wawakilishi wa wananchi waliojitolea kuendesha kesi ya bomoa bomoa katika jimbo la Segerea, ambapo Mahakama kuu divisheni ya ...

Baadhi ya wawakilishi wa wananchi waliojitolea kuendesha kesi ya bomoa bomoa katika jimbo la Segerea, ambapo Mahakama kuu divisheni ya Ardhi kufutilia mbali uamuzi wa wananchi hao. 
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye chumba cha maamuzi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanachi wa Jimbo la Segerea wakiwa nje ya Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi jijini Dar es Salaam leo wakimsikiliza Katibu wa Kamati ya Jimbo la Seerea, Ramadhan Mwani (Katikati aliyenyoosha mkono)mara baada ya Mahakama hiyo kuifuta Kesi ya Bomoa bomoa ya Jimbo la Segerea.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imetupilia mbali kesi ya walalamikaji waliojenga maeneo hatarishi kwa maisha ya binadamu katika jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa kukosa baadhi ya majina ya walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imetupilia kesi ya wakazi 2619 ya kupinga kubomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote na serikali kwa wakazi zaidi ya elfu nne wa eneo hilo mara baada ya wakazi hao kukosa majina na sahihi za wananchi walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Jaji Fredrica Mgaya wakati shauri hilo amesema kesi hiyo imefutwa kwa kukosa majina na sahihi za watu wanaotaka kuwakilishwa na watu wanane walioshauriana kuwa watawasimamia katika kesi hiyo ya bomoabomoa ya wakazi wa jimbo la Segerea.

Akisoma maamuzi ya  wakili wa serikali Gabriel Malata amesema kuwa walalamikaji hawana kibali au viapo halali vya wakazi hao kuomba kuwakilishwa na watu walioteuliwa kuwasimamia katika kesi yao ya kubomolewa makazi yao.


Pia Jaji Fredrica Mgaya ameiomba  serikali kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni ili wajue athari zitakazo wakuta kutokana na mabadiliko y hali ya hewa.

Related

kitaifa 2128630255744012740

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item