Fastjet yatoa ofa nauli za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza | LUKAZA BLOG

Fastjet yatoa ofa nauli za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Dar es Salaam, 12 Aprili 2016 -Shirika la ndege la bei nafuu, fastjet, limetangaza punguzo la nauli...


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, 12 Aprili 2016-Shirika la ndege la bei nafuu, fastjet, limetangaza punguzo la nauli la sh. 22,000/- kwa mwezi huu wa Aprili kwenye safari zake za Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza.

Kulingana na Afisa Masoko na Uhusiano wa Umma wa fastjet, Lucy Mbogoro, ofa hiyo ijulikanayo kama JET10 imeanza kuanzia mwanzo wa April na itamalizika tarehe 30 Aprili 2016.

“Ofa hii kutoka fastjet inaashiria kwa mara nyingine tena jinsi shirika letu linavyosikiliza matakwa ya wateja wake”, alisema Mbogoro.

Mbogoro alisema kwamba wateja wanaweza kilipia nauli zao kupitia mitandao ya Tigo-Pesa, Airtel Money, M-Pesa and pia kupitia NMB Mobile Cash katika tawi lolote la Benki ya NMB.

“Wateja wanashauriwa kukata tiketi mapema ili kufurahia nauli za bei nafuu zaidi na pia wanaweza kulipia kupitia m.fastjet.com or www.fastjet.com.” alishauri Mbogoro.

Related

Biashara 4047133743342424913

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item