GARI LATUMBUKIA BAHARINI ENEO LA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM, WALIOKUWEMO WAHOFIWA KUFA | LUKAZA BLOG

GARI LATUMBUKIA BAHARINI ENEO LA FERRY JIJINI DAR ES SALAAM, WALIOKUWEMO WAHOFIWA KUFA

NA K-VIS MEDIA –Kigamboni Ferry GARI aina ya Hiace limetumbukia baharini eneo la Ferry jijini Dar es Salaam mapema leo alfajiri Aprili ...

NA K-VIS MEDIA –Kigamboni Ferry
GARI aina ya Hiace limetumbukia baharini eneo la Ferry jijini Dar es Salaam mapema leo alfajiri Aprili 20, 2016 na habari zisizo rasmi zinasema watu wawili mwanamke na mwanamme wanahofiwa kufa maji.
Mashuhuda wanasema, wapiga mbizi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ, kikosi cha navy, wamefanikiwa kuopoa mwili wa mwanamume na kazi ya kutafuta maiti ya mwanamke inaendelea. Mashuhuda wanasema, Hiace hiyo ilitumbukia baharini kutoka kwenye kivuko (Ferry) na sababu za kutumbukia kwa gari hilo bado hazijajulikana. Polisiinaendelea na uchunguzi.
Boti ya mwendo kasi ya JWTZ, ikiwa na wazamiaji imeonekana eneo la mpwani ya magogoni ikiwa kwenye kazi ya kuwatafuta wahanga na gari hilo


Related

Hot Stories 8987131066932785343

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item