Habari za Hivi Punde: Alshabab wavamia kituo cha polisi Wajir Kenya | LUKAZA BLOG

Habari za Hivi Punde: Alshabab wavamia kituo cha polisi Wajir Kenya

Image copyright AFP Image caption Alshabab wavamia kituo cha polisi Wajir Kenya Wapiganaji takriban 100 wa kundi la kigaidi la Alshabab...

Image copyrightAFP
Image captionAlshabab wavamia kituo cha polisi Wajir Kenya
Wapiganaji takriban 100 wa kundi la kigaidi la Alshabab wamevamia kituo kimoja cha polisi Wajir Kaskazini mwa Kenya.
Hadi kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ama kufa haijajulikana lakini kinachothibitishwa na serikali kuwa walifaulu kuteka gari la serikali aina ya Land Cruiser.
''wavamizi walishambulia kituo cha polisi cha Diff na wakakabiliwa vikali na askari waliokuwepo, wengi wao walijeruhiwa ila walifaulu kuteka nyara gari la serikali la kituo cha Diff ambalo walitumia kuwabeba majeruhi wao'' alisema Inspekta Jenerali wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet.
Maafisa 3 wa polisi wa Kenya walijeruhiwa.
Kundi hilo lilitorokea mpakani.
Kikosi cha jeshi la Kenya limewafuata huko baada yao kuvuka mpaka kati ya Kenya na Somalia.Chanzo BBC swahili

Related

Kimataifa 1367881744802468150

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item