KAJUNASON ASHEREKEA SIKU YAKE ZA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA SOS CHILDREN'S VILLAGE TANZANIA | LUKAZA BLOG

KAJUNASON ASHEREKEA SIKU YAKE ZA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA SOS CHILDREN'S VILLAGE TANZANIA

 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (mwenye shati nyeupe) akimkabidhi mwakilishi wa kituo cha SOS Children's Village Ta...


 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (mwenye shati nyeupe) akimkabidhi mwakilishi wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania Bi. Sherry Mavura (wa kwanza kulia) msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo Sabuni, Unga, Mchele, Mafuta, miswaki, dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia kuendesha kituo hicho.

"Leo mchana Aprili 10, 2016 nimesherekea siku yangu ya kuzaliwa na kutimiza miaka 10 ya Uandishi wa Habari na watoto Yatima wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar kwa kula nao chakula, kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapa msaada wa vitu mbali mbali. Nawashukuru wale wote walioungana na mimi. Mungu awabariki sana" alisema Kajuna.
 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akiwagawia juisi watoto yatima wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwenye  kituo cha kulelea  watoto yatima cha kituo cha SOS Children's Village Tanzania.
Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna pamoja na mwenyekiti wa Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw. Joachimu Mushi wakiwa kwenye pozi na watoto. Mwenyekiti wa TBN ni mmoja ya wageni waalikwa waliosindikiza.
Cathbert Angelo Kajuna kiimbiwa wimbo na familia yake pamoja na baadhi ya watoto yatima wakati wa ukataji keki aliyokula na watoto hao katika kituo cha ha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar.
Cathbert Angelo Kajuna akiwalisha baadhi ya watoto yatima siku yake ya kuzaliwa kwenye  kituo cha SOS Children's Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar
Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki rafiki yake Imani Ntila.
Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki mwenyekiti wa Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw. Joachimu Mushi.
Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki mwakilishi wa kituo cha SOS Children's Village Tanzania Bi. Sherry Mavura.
Watoto wakipewa zawadi.
Picha ya pamoja.

Related

kitaifa 6851001152533978184

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item