Kama wewe ni mpenzi wa filamu za Action basi hii ndio kosa lililoonekana katika Filamu ya "London Has Fallen" | LUKAZA BLOG

Kama wewe ni mpenzi wa filamu za Action basi hii ndio kosa lililoonekana katika Filamu ya "London Has Fallen"

Baadhi ya vipande vya filamu ya London Has Fallen. Filamu ya London Has Fallen ni moja kati ya filamu za kimarekani iliyotoka mwaka h...

Baadhi ya vipande vya filamu ya London Has Fallen.
Filamu ya London Has Fallen ni moja kati ya filamu za kimarekani iliyotoka mwaka huu 2016 mwezi wa tatu tarehe 4 kutoka kwa Kampuni ya Focus Features chini ya lebo yao mpya ya Gramercy Pictures.

Filamu hii imeongozwa na muongazaji aitwaye Babaki Najafi huku stori yake ikiwa imeandikwa na Creighton Rothenberger, Katrin Benedikt, Chad St. John, and Christian Gudegast. Filamu hii ya London Has Fallen ni mfuatilizo wa filamu ya Antoine Fuqua iliyotoka mwaka 2013 ijulikanayo kama Olympus Has Fallen huku stars wa filamu hii ya London Has Fallen wakiwa ni Gerard ButlerAaron Eckhart, and Morgan Freeman, with Alon Moni AboutboulAngela BassettRobert ForsterMelissa Leo,Radha Mitchell and Charlotte Riley huku wakimsaidia muhusika mkuu.

Filamu hii ya London Has Fallen ilianza kutengenezwa kwa mara ya kwanza tarehe 24 October 2014 huko London huku mapumziko ya Sikukuu ya Noel (Christimas) yanayoanza mwezi november kuwa sababu ya kusitisha kutengenezwa kwa filamu hiyo ambapo February 2015 utengenezaji wa filamu hiyo uliendelea na mnamo mwaka 2016, March 4 filamu hii ikazinduliwa rasmi.

Katika Filamu hii inayomuonyesha Rais wa Marekani akiwa katika hali ngumu ya kukabiliwa na kutekwa na kujaribu kuuliwa ndipo Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais Special Agent Mike Banning (Gerard Butler) alipopambana kufa na kupona kwaajili ya kumuoka rais wa Marekani ambae alitekwa na magaidi mara baada ya mashambulizi yaliyotokea wakati viongozi mbalimbali wa nchi za amerika walipokwenda London kuhudhuria Mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza James Wilson.

Mara baada ya Rais wa Marekani kupokea taarifa ya kifo cha waziri mkuu wa Uingereza Bw James Wilson ndipo akasafiri kuelekea London kwaajili ya kuhudhuria mazishi akiongoza na msaidizi wake Lynne Jacobs (Angela Bassett) pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais Special Agent Mike Banning (Gerard Butler). Wakati viongozi mbalimbali wa nchi nyingine wakiwasili katika msiba huo sekeseke la magaidi likaanza na ndipo magaidi wakafanya shambulio hatari sana chini ya amri ya kiongozi wao Barkawi, shambulio hilo lililosababishwa na  bomu lililofanikiwa kuwekwa chini ya Gari la waziri mkuu wa Canada na moja wa magaidi aliyejifanya ni Askari Polisi wa Uingereza na kufanikiwa kulipuka na kumuua Waziri Mkuu wa Canada Bw Trafalgar Square pamoja na mke wake. Viongozi wengine walipatwa na majanga ya kupoteza maisha katika hali matukio tofautitofauti huku Kansela wa Ujerumani na walinzi wake wakiuliwa na magaidi hao wakati wakiwa wamesimama wakishuhudia msafara wa Makamu wa Rais wa Canada ukiingia.

Wakati wa shambulizi hilo kutokea ndipo magaidi wakaanza kurushiana risasi na Walinzi wa Rais wa Marekani huku magaidi wakiwa ndani ya sare za askari wa uingereza na watu wa huduma ya kwanza, katika mashabulizi yalisababisha wengi kupoteza maisha Rais wa Marekani pamoja na Msaidizi wake Lynne Jacobs na Mlinzi wake Special Agent Mike Banning (Gerard Butler) wakafanikiwa kutoroka.

Wakati wakitoroka kurejea kwenye Helikopta ya Rais ijulikanayo kama Marine One kwaajili ya kuondoka , Magaidi wakiwa katika kambi yao ya operation walifanikiwa kudukua mtandao wa Umeme wa jiji na kufanikiwa kuzima umeme katika jiji lote. Mara baada ya Rais wa marekani kufika katika Marine one ambayo ilikua na escoti ya heliktopa mbili zilifanikiwa kuruka na kuanza safari ya kurudi Marekani lakini kwa bahati mbaya magaidi walikuwa juu ya Maghorofa walianza kuzitungua ndege hizo kabla ya kuitungua marine one.  

My Critic baada ya kuingalia filamu hii nimeweza kuona kuwa wakati wa Rais wa marekani na msaidizi wake wakitoroka kutoka katika viwanja vya Buckingham Palace walitumia gari aina ya Land Rover Discovery ambapo kwa utaratibu wa matumizi ya magari ya rais ambayo tunafahamu kuwa rais wa Marekani huwa anatumia gari aina ya Cadillac One ambalo lipo vizuri sana hasa wakati wa mashambulizi na ni moja ya gari ambalo haliingizi risasi wala bomu sasa katika hili wameshindwa kutuonyesha rais akitumia gari hilo wakati wa kutoroka kutoka kwenye mashambulizi hayo na kutuonyesha akitumia gari nyingine kitu ambacho kwa utaratibu wa rais wa marekani huwa tunaona gari lake la Cadillac One likitumika kwaajili ya vitu kama hivyo.

Katika kipande hiko wameshindwa kwasababu Mwanzo walifanikiwa kutuonyesha Usafiri wa Rais katika Ndege ambapo Ilionyeshwa ndege ya Rais Air Force one , na wakafanikiwa kutuonyesha Cadillac One wakati akielekea kwenye viwanja vya Buckingham Palace lakini wakashindwa kutuonyesha  gari hilo likitumika wakati wakitoroka kwenye mashambulizi . Inawezekana wamefanya hivyo kwasababu za kibiashara kutokana na gari aina ya Land Rover Discovery kutumika badala ya gari ya Cadillac One. 

Mwisho wa Yote ni filamu moja nzuri yenye kusisimua ambapo Kazi ya Cinematrographer imeweza kuonekana katika filamu hiyo. Kama hujaiangalia filamu hiyo basi itafute na uitazame na wewe utuambie mtazamo wako katika filamu hii.


UNAHITAJI STORY ZAIDI?
 Tufollow katika Facebook Lukaza Blog, Insta:LukazaBlog, Twitter: Lukaza2010 na Youtube MultiLukaza Blog kwa kupata habari motomoto na latest kuhusu filamu, tv na muziki na mengineyo.


Kama imekukuna unaweza share na washikaji zako popote pale iwe Facebook, Twitter, Instagram na Hata Kwenye Whatsapp

Related

Makala 4539079335948193917

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item