MFANYABIASHARA ZA MAGENDO ATUMBULIWA JIPU NA TRA | LUKAZA BLOG

MFANYABIASHARA ZA MAGENDO ATUMBULIWA JIPU NA TRA

Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo ak...

Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.
Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Na Mwandishi Wetu-Kilwa.
Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST)  wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh.

Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu.

Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko 762 Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135, Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49, Betri aina ya tigger katoni 223, Amira katoni 135, Sabuni za kufulia katoni 48

Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari. Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini vya sukari vya Kilombero, TPC na Mtibwa Sugar.
Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India  2000 Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari 36,000 mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo 25 kiasi cha 1150 Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609 Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Nyumba hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo hutumika kuweka bidhaa kabla ya kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.
sehemu ya kuweka sukari na kupima.
Nyumba inayotumika kuweka sukari
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA
 
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni
Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.
Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta
Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda.

Related

Hot Stories 6879388149198019573

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item