MRADI WA KAIZEN KUTOKA JAPAN KUKUZA UZALISHAJI NA UBORA WA BIDHAA NCHINI | LUKAZA BLOG

MRADI WA KAIZEN KUTOKA JAPAN KUKUZA UZALISHAJI NA UBORA WA BIDHAA NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akizungumza na kukaribisha Ujumbu wa Wataalamu kutoka nchini Japani katika mradi wa u...

MW1
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akizungumza na kukaribisha Ujumbu wa Wataalamu kutoka nchini Japani katika mradi wa ushauri wa kuwekeza katika Rasirimali watu na vitendeakazi ili kuzalisha kwa tija na ubora wa bidhaa kupitia mradi wa KAIZEN ili kuwekeza zaidi kwa namna unavyozalisha na kufanya kazi kwa tija, wakati wataalamu hao walipokutana na Waziri huyo wataalamu mbalimbali wa Wizara ya Viwanda na Biashara katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo mwishoni mwa wiki.
Waziri Mwijage amesema wataalamu hao wanashauri mambo mengi katika uzalishaji wa bidhaa na kilimo kama vile kuwapa uelewa zaidi wataalamu na wajasiriamali wenyewe ili kuwekeza katika viwanda na kilimo kwa tija na ubora ili kufikia malengo ya kuwafanya watu kuwekeza kwa tija na ufanisi, Ukielewa namna nzuri ya uwekezaji wenye tija na ubora utaweza kufaidika na uwekezaji wako bila kutumia nguvu na gharama kubwa sana bila mafanikio.
Katika picha kulia ni Profesa Tetsushi Sonobe Makamu wa rais wa Shirika la GRIPS la Japan na katikati ni Profesa Toshio Nagase Mwakilishi wa shirika la JICA nchini Tanzania.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
MW7
Profesa Toshio Nagase Mwakilishi wa shirika la JICA nchini Tanzania akitoa utambulisho wa ujumbe aliofuatana nao katika mkutano huo uliofanyika katika Wizara ya Viwanda na Biashara mwishoni mwa wiki.
MW6
Profesa Tetsushi Sonobe Makamu wa rais wa Shirika la GRIPS la Japan akiwasilisha maelezo ya mradi huo kwa wataalamu wa Wizara ya Viwanda na biashara.
MW5
Bw. Takao Kikuchi Mshauri Mkuu wa mradi wa KAIZEN nchini akichangia jambo katika mkutano huo uliohudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka wizara ya viwanda na biashara na Japan.
MW4
Wataalamu mbalimbali kutoka Shirika la Maendeleo la Japan JICA na Mradi wa KAIZEN wakifuatilia mazungumza katika mkutano huo.
MW3
Wataalamu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Japan wakati mkutano huo ukiendelea.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akizungumza kwa msisitiza wakati alipokuwa akielezea mambo mbalimbali kuhusu mradi wa KAIZEN unaoendeshwa na wataalamu kutoka nchini Japan.

Related

Kijamii 8434919391241251387

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item