Rais Museveni: Mradi Bomba la Mafuta ghafi, utapita Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga | LUKAZA BLOG

Rais Museveni: Mradi Bomba la Mafuta ghafi, utapita Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga

Leo Tarehe 23 Aprili, 2016 Tanzania yafanikiwa kupata Bomba la mafuta ghafi baada ya Mhe. Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda kutoa kauli y...


Leo Tarehe 23 Aprili, 2016 Tanzania yafanikiwa kupata Bomba la mafuta ghafi baada ya Mhe. Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda kutoa kauli ya mwisho Kuwa Mradi Bomba la Mafuta ghafi utapita Njia Kaskazini mwa Tanzania hadi Bandari ya Tanga.

Kauli hiyo imetolewa Leo Saa 7 mchana katika mkutano wa 13 wa Northern Corirodor uliofanyika Munyonyo Nje Kidogo ya Jiji la Kampala. Kauli hiyo ilitolewa mbele ya marais wa Kenya, Rwanda, na Wawakilishi wa South Sudan, Ethiopia, Tanzania, DRC na Burundi.

===============


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa kuhusu Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Tanga hadi Uganda


Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.

Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda.

Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa

Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, 
Dar es Salaam
23 Aprili, 2015

===============

“I have agreed with President Uhuru Kenyatta that let the two pipelines go ahead."

[​IMG]
President Museveni speaking at the 13th Northern Corridor Intergration Projects Summit in Kampala on Saturday. (Credit: PPU)

KAMPALA - It’s signed and sealed. Uganda’s crude oil pipeline from Hoima will pass through the Tanzanian port of Tanga, President Yoweri Museveni announced on Saturday.

The announcement ends weeks and months of expectation and anxiety around one of the most critical projects in Uganda’s oil development journey 10 years since oil was first discovered in Uganda.

“I have agreed with President Uhuru Kenyatta (of Kenya) that, let the two pipelines go ahead, one from Lokichar to Lamu and another from Hoima to Tanga,” said Museveni.

This was at the closure of the 13th Northern Corridor Infrastructure Projects in Munyonyo.
[​IMG]
[​IMG]
[​IMG]
[​IMG]
[​IMG]

Related

Hot Stories 100083105027300919

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item