TANAPA YAZINDUA KAMPENI KILIMANJARO YENYE KAULIMBIU “ WEKA MLIMA SAFI, TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE” | LUKAZA BLOG

TANAPA YAZINDUA KAMPENI KILIMANJARO YENYE KAULIMBIU “ WEKA MLIMA SAFI, TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE”

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjarom iliyokuwa na kaulimb...

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjarom iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze” katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki.
Wakurugenzi kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo, Mkurugenzi wa Mipango Dk. Ezekiel Dembe, Mkurugenzi wa Fedha Nassoro Mndeme na nyuma yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori  Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima  Kilimanjaro.
Baadhi ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau kutoka Kampuni mbalimbali za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaoshiriki Kampeni maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Idadi kubwa ya wadau wa sekta ya utalii walishirikiana vema na TANAPA kusafisha Mlima Kilimanjaro.
Wageni waalikwa wakivaa ‘gloves’ kabla ya kuanza zoezi la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima  Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mazingira safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi. Na Dixon Busagaga waGlobu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Related

Hot Stories 4141099194185364702

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item