Kijana mmoja mkazi wa Buguruni Kisiwani ametiwa mbaroni na uongozi wa mtaa huo baada ya kubainika kuwa na kuku 78 waliokufa ambao alikuwa akiwaandaa tayari kuwasambaza kwa wauza chips jijini Dar es Salaam.
Ally Ibrahim amekamatwa leo asubuhi baada ya taarifa kutoka kwa wasamaria wema kutoa taarifa kwa uongozi wa mtaa kuwa ndani ya nyumba moja huwa waatengeneza kuku waliokufa na kuwauza kwa watengeneza chips na watu huwatumia wakiamini ni chakula salama.
Baba na mama wa familia hiyo walifanikiwa kutoroka kabla ya kutiwa mikono mwa serikali.
Mwenyekiti wa mtaa amesema kuwa alikuta kuku hao wakiandaliwa ambapo watuhumiwa huwanunua kuku wakiwa tayari wamekufa na kuwaandaa kisha kusambaza kwa ajili ya watu kuwatumia.
Aidha, akizungumza fisa afya wa kata amebaini kuwa kuku hao hawafai kwa matumizi ya binadamu na ameagiza wateketezwe mara moja ili kuepushwa mlipuko wa magonjwa.