Alikiba amuombea kura Msanii Diamond Platnum | LUKAZA BLOG

Alikiba amuombea kura Msanii Diamond Platnum

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda  mfupi ni sawa na kuc...


Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda  mfupi ni sawa na kuchana msamba kwa maana siyo hatua za kawaida.

Alikiba alisema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo ambacho kinarushwa na kituo cha  East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya ‘Sony Music’ ni jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.
“Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki waliupokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na ‘Sony Music’ ndani ya muda mfupi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida” alisema Alikiba.
Mbali na hilo Alikiba alimuombea msanii Diamond Platnum kwa watanzania ili wampigie kura kwenye tuzo anazoshiriki sasa na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
Chanzo: Eatv.tv

Related

Hot Stories 5458375079672790657

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item