Bob Chacha Wangwe alivyobadili gia angani | LUKAZA BLOG

Bob Chacha Wangwe alivyobadili gia angani

Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha ta...

Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha
Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na  Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.

Mtoto huyo, Bob Chacha  Wangwe (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  alibadili msimamo jana aliposomewa shtaka hilo kwa mara ya pili, katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wangwe alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 11, na alisomewa shtaka linalomkabili na alikiri kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa anapokiri kosa, kwa kawaida Mahakama inaweza kumtia hatiani na kumpa  adhabu kwa mujibu wa sheria, kulingana na kosa siku hiyo hiyo au siku  nyingine yoyote.

Baada ya kusomewa shtaka na kukiri, Hakimu  Mkazi Mkuu, Waria lwande Lema, aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe rumande  hadi jana, Mei 17, kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo  hakuwapo.

Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alipopandishwa  kizimbani na kusomewa shtaka hilo, ili kusomewa maelezo ya awali kabla  ya Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu, tofauti na siku ya kwanza,  alikana kutenda kosa hilo.

Kutoka na mshtakiwa huyo kukana kosa, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, aliieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa  kesi hiyo.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala aliiomba  Mahakama impe dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika,  maombi ambayo yalikubaliwa na aliachiwa kwa dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 15.

Wangwe ambaye baba yake kwa sasa ni marehemu,  anadaiwa Machi 15, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo  kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Related

Hot Stories 2893782746609397746

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item