Huawei Kuwa Kinara wa Simu za Kisasa Tanzania 2016 | LUKAZA BLOG

Huawei Kuwa Kinara wa Simu za Kisasa Tanzania 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang, akitoa hotuba kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka la Huawei li...

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang, akitoa hotuba kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala akitoa hotuba kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala(kushoto) aliyekuwa mgeni rasimi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam akikata utepe wa duka hilo katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang.
Bw. Sylvester Manyara,  Mkurugenzi mkuu wa mauzo na usambazaji wa Huawei Devices Tanzania (kushoto) akimuonyesha baadhi ya simu mpya za Huawei Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala aliyekuwa mgeni rasimi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang, na wa pili kulia ni Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania.
Uongozi wa kampuni ya Huawei Devices Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Bw. Sylvester Manyara,  Mkurugenzi mkuu wa mauzo na usambazaji wa Huawei Devices Tanzania (kushoto) akimuonyesha baadhi ya simu mpya za Huawei Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala(Kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Dar es Salaam, Mei 2016: Huawei Tanzania imeendelea kubuni mbinu mpya za kukidhi haja za wateja wake kwa kuwaletea karibu simu na vifaa vyenye viwango vya kimataifa. Ili kuwahudumia wateja wake katika namna bora na ya ufanisi Zaidi. Kampuni ya Huawei Tanzania wamezindua duka lake la 6 hapa City Mall, Dar es Salaam; ikiwa ni hatua ya kuitikia uhitaji mkubwa wa vifaa vya Huawei nchini na kuhakikisha kuwa bidhaa halisi na huduma bora za Huawei zinapatikana kwa wateja kwa urahisi.

Hili ni duka la tatu la bidhaa hii katika jiji la Dar es Salaam, huku maduka mengine yakiwa yamezinduliwa katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya. Duka hili limekusudiwa kuleta hisia na mguso wa bidhaa za Huawei kwa wateja, na kuboresha kiwango cha huduma azipatazo mteja jijini.
Huawei Tanzania imejizatiti kuwa kinara katika bidhaa zya kisasa na zenye ushawishi zaidi Tanzania, kwa kuwapatia wateja simu zenye matumizi rafiki.  Kampuni hii imedhamiria kuwa kinara wa bidhaa ya simu za kisasa Tanzania mwaka 2016. Kwa sasa Huawei Tanzania imeshika nafasi ya pili, ikiwa na hisa za soko za 22% kwa mujibu wa takwimu za robo ya kwanza ya mwaka 2016.

Akizungumzia kuhusiana na mkakati wa Huawei Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania, Ndg. Bruce Zhang amesema kuwa mwaka huu kampuni ya Huawei Tanzania imekusudia kuongeza wigo wa usambazaji Tanzania, ikilenga mikoa ya kanda ya Ziwa, kanda ya Kaskazini, kanda ya Kusini na kanda ya Kati.

“Tunampango wa kuongeza wigo wetu kutoka mawakala 250 tulio nao sasa mpaka kufikia mawakala 700, tunalenga kuwa na maduka 10 ya Huawei, maduka 20 ya mawakala wakubwa, 500 ya mawakala  wa rejareja. Kampuni ya Huawei Tanzania imedhamiria kufikia 90% ya Tanzania.” Alithibitisha Mkurugenzi Mtendaji.

Kutokana na maduka haya, Huawei Tanzania inatazamia idadi kubwa ya watanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

Akiongea na washiriki wakati wa uzinduzi, Mh. Raymond Mushi mkuu wa wilaya ya Ilala, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema, “ufunguzi wa duka la tatu la Huawei Tanzania hapa Dar es Salaam, ni udhihirisho wa kuongezeka kwa dhamira ya Huawei Tanzania kwa jamii.” Mh. Raymond Mushi pia aliipongeza Huawei Tanzania kwa hatua iliyochukua hivi karibuni ya kutambua mchango za mawakala katika mikoa yote na kuwatunuku vyeti pamoja na kuanzisha mpango wa motisha kwao.

Teknolojia imeendelea wakati wote kuchukukua nafasi muhimu ya jinsi tunavyowasiliana. Mawasiliano ya wanadamu yameendelea kubadilika kipindi hadi kipindi katika karne kadhaa. Huawei Tanzania imeleta vifaa vyenye teknolojia ya juu kabisa kama vile P9, Mate 8, GR5, GR3, Y6pro, Y3C, and Y3 Lite ili kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na uwanja mpana wa machaguo yao.

Akizunguzia kuhusu vifaa vipya vilivyoingizwa katika soko la Tanzania Bw. Zhang alisema “Msukumo wetu kwa wateja huenda mbali zaidi ya ubora wa bidhaa, kila ubunifu wa Huawei hutokana na ushirikishwaji wa wateja wetu na kuelewa mahitaji yao na uhitaji wa soko”
Katika kusherehekea ufunguzi wa duka hili la bidhaa za Huawei lililopo City Mall, Huawei Tanzania inatoa ofa ya punguzo maalumu la simu kuanzia tar. 14 hadi 20 Mei sambamba na zawadi mbalimbali zikiwemo fulana, spika zenye Bluetooth, na vifaa ya kusikilizia muziki masikioni vyenye Bluetooth pia.

Hivi karibu Huawei Tanzania imedhamiria kufungua maduka mengi zaidi na vituo vya simu vya huduma kwa wateja nchi nzima ili kuwahakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma bora na vifaa halisi vya Huawei na pia kutoka fursa nyingi zaidi za ajira kwa watanzania.

Huawei inatambua ushirikiano inaoupata kutoka kwa serikali ya Tanzania kwa miaka mingi sasa, kwa kuthibitisha dhamira ya Huawei katika upatikanaji wa vifaa orijino na kushiriki katika mkakati wa serikali kupitia kampeni ya TCRA ya kuondosha simu feki Tanzania. Huawei Tanzania inaendelea kuwaletea bidhaa orijino karibu zaidi kwa watumiaji wake kwa kufungua maduka yake nchi nzima na zaidi ya yote, tumeanza kutoa vyeti vya uthibitisho vya Huawei Tanzania kwa mawakala ili kujiridhisha kuwa wanauza vifaa na simu halisi za Huawei.

Kuhusu Huawei
Huawei huongoza duniani katika Teknologia ya Mawasiliano. Ikibuni wakati wote kwa kuzingatia mahitaji ya wateja, wamejikita katika kuongeza uzoefu wa wateja na kuleta thamani ya juu kwa mashirika ya simu, makampuni na wateja. Vifaa vya mawasiliano ya simu ya Huawei, bidhaa za Teknologia ya Mawasiliano, na simu za kisasa hutumika katika nchi 170 ulimwenguni. Huawei ipo nafasi ya 3 katika usambazaji wa simu  (2015) ilikiwa imesambaza zaidi ya simu milioni 110 ulimwenguni. Huawei Tanzania imedhamiria kuwa kinara katika bidhaa borana za kisasa ulimwenguni, ikiwa inatoa huduma za simu internet rahisi zaidi kutumiwa na wateja. Kwa sasa, Huawei Tanzania ipo nafasi ya 2 ikiwa na hisa za soko la 22% (katika robo ya kwanza ya mwaka)  


Hotuba ya  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
Wadau wetu mbalimbali.
Wafanya biashara wenzetu.
Wawakilishi kutoka vyombo vya habari
Mabibi na Mabwana

Alasiri ya leo, tunaadhimisha historia ya muhimu kutoka kampuni ya Huawei Tanzania. Kwa unyenyekevu mkubwa, ninayo furaha kuwakaribisheni ninyi nyote katika tukio hili maalumu la uzinduzi wa duka la Huawei katika jengo la City Mall.

Kwa kuongozwa na uhitaji mkubwa wa wateja, kampuni ya simu ya Huawei Tanzania kwa ufanisi mkubwa, imeendelea kuzindua njia mpya za kuwahudumia wateja wake kwa ubora zaidi ili kuwapatia huduma zenye viwango vya kimatafa na kutatua matatizo yao ya vifaa vya kieletroniki. Uzinduzi huu unatuongezea  duka la tatu kwa hapa Dar es Salaam kufuatia maduka mawili yaliyozinduliwa mwishoni mwa mwezi Februari Dar, na mengine yakiwa yamezinduliwa mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya. Hatua hizi ni mwitikio katika ukuaji wa uhitaji wa simu za Huawei jijini na kuhakikisha simu orijino za Huawei zinapatikana kwa wateja. Duka hili linadhamiria kuleta mguso na hisia pekee kwa watumiaji wote wa bidhaa za Huawei, pamoja na kuboresha kiwango cha ubora wa ujuzi kwa wateja hapa jijini.

Nina Imani kubwa kwamba duka la Huawei la City mall litakuwa na matokeo bora kwa kuwa na mauzo mazuri na huduma bora kama tulivyoona katika yale maduka mengine.

Mabibi na Mabwana
Kampuni ya simu ya Huawei Tanzania imejikita katika kutengeneza simu bora na zenye mvuto zaidi hapa Tanzania, simu ambazo ni rafiki kwa watumiaji wote. Tumejiwekea mikakati na mipango madhubuti kuwa kinara namba moja kwenye matoleo bora za simu hapa Tanzania mwaka 2016. Kwa sasa kampuni ya Huawei Tanzania ni ya pili, ikiwa na hisa za soko la 22% kwa takwimu za robo ya kwanza ya mwaka 2016.

Mwaka huu tunajipanga kupanuka zaidi na kusambaa Tanzania, hasa kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini, kanda ya kusini, pamoja na kanda za kati. Pia tunadhamiria kuongeza kasi yakufikia mawakala wengi zaidi kutokea 250 waliopo hadi 700, kuwa na maduka 10 ya Huawei, na maduka 20 ya mawakala wakubwa, na mawakala 500 wa rejareja. Kampuni ya Huawei Tanzania imepanga kusambaa kwa Zaidi ya 90% nchini Tanzania.

Mabibi na Mabwana
Tunatambua msaada kutoka serikali ya Tanzania kwa miaka kadhaa sasa, kuhimiza jitihada za Huawei katika kutoka vifaa orijino na kushirikiana na  serikali kupitia TCRA kwenye harakati za kutokomeza simu feki Tanzania. Huawei Tanzania inazidi kuongozea ufanisi wa upatikanaji wa bidhaa orijino kwa watanzania kwa kufungua maduka nchini kote, na kwa sasa tunatoa vyeti kwa mawakala wetu kuhakikisha kuwa wanauza simu za kisasa orijino kutoka Huawei.

Mabibi na Mabwana

Huawei imetajwa kuwa kinara kwenye tuzo za bidhaa bora ulimwenguni kwa mwaka 2014 na 2015. Kwa mujibu wa ripoti, thamani ya bidhaa ya Huawei, inakadiriwa kuwa dola za kimarekani bilioni 5 kwa mwaka 2015, ongezeko la 15% ulikinganisha na mwaka 2014. Huawei pia imetajwa kuwa miongoni mwa kampuni zinazokua kwa kasi katika sekta ya teknolojia. Kuwa namba 3 kwenye oridha ya wauzaji wa simu ulimwenguni, Huawei imeongeza mauzo na mapato kwa 80% kwa kufikia bilioni 22 kwa mwaka 2015. Usambazaji wa simu za Huawei pia nao umeongezeka kwa 45% mwaka jana, kusambaza zaidi ya simu milioni 110 ulimwenguni kote.

Huawei pia imeng’ara kwenye listi ya bidhaa zenye ubora duniani maarufu kama BRANDZ “Top 100 Most Valuable Global Brands ‘ kwa mwaka 2015”. Huawei ni kampuni ya kwanza kutoka china kuwa kwenye orodha mbili kwa mpigo, kwa  BRANDZ na INTERBRAND kwa mwaka 2015. Mwaka huohuo Huawei iliorodheshwa katka nafasi ya 88 katika tuzo za Inter brand “kampuni 100 zenye bidhaa bora” kwa mwaka 2014 Huawei pia imetajwa na mtandao wa linkedln kama “kampuni 100 zinazopendwa na waajiriwa duniani”

Tuna uhakika kwamba kwa ushirikiano na wadau wetu Tanzania tutaendelea kukuza maendeleo hayo na kuendelea kusaidia kutengeneza kesho iliyong’ara.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala
Mabibi na Mabwana
Kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wa kampuni ya Huawei Tanzania, napenda kuwashukuru wote kwa kujitoa kwenu na kufanikisha tukio letu hili muhimu.
Asanteni. 

Related

Hot Stories 3430650414034266220

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item