Mahakama yatupilia mbali rufaa ya DPP kuhusu kesi ya Kitilya na wenzake | LUKAZA BLOG

Mahakama yatupilia mbali rufaa ya DPP kuhusu kesi ya Kitilya na wenzake

Leo Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka(DPP)dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri...

Leo Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka(DPP)dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.

Jumanne wiki hii Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisema kuwa jalada la kesi inayowakabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Msamire Kitilya na wenzake kimsingi bado lipo Mahakama Kuu na kwamba washtakiwa hao walitakiwa kwenda mbele ya Jaji Mfawidhi kwa maelekezo mengine.


Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru pale kesi ya washtakiwa hao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya mawakili wa pande zote mbili kusema ya kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kupata maelekezo kutoka Mahakama Kuu kama ilivyoamuliwa mara ya mwisho.

Related

Hot Stories 8748282368561790983

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item