Mhandisi ashauri kufanyike uwekezaji wenye kuleta mapinduzi nchini , Asema TBL Group inatekeleza miradi ya kunufaisha jamii | LUKAZA BLOG

Mhandisi ashauri kufanyike uwekezaji wenye kuleta mapinduzi nchini , Asema TBL Group inatekeleza miradi ya kunufaisha jamii

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakishiriki shughuli za kijamii za kusafisha mazingira   Mhandisi Richmond Raymond akiangalia pumba za m...

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakishiriki shughuli za kijamii za kusafisha mazingira
 Mhandisi Richmond Raymond akiangalia pumba za mpunga ambazo ni malighafi katika kiwanda cha Mwanza
Mhandisi Richmond Raymond


Meneja wa kiwanda cha Bia ya bia cha TBL cha mjini Mwanza,Mhandisi Richmond Raymond ameshauri kuwa ili taifa la Tanzania liondokane na tatizo la umaskini kwa haraka wawekezaji katika sekta zote wanapaswa kulenga pia kusaidia jamii zilizowazunguka na kuwa na mtazamo wa kunufaisha watu wengi zaidi kutokana na uwekezaji huo.
Katika mada yake aliyoitoa hivi karibuni katika mkutano wa masuala ya  Uwekezaji wa kustawisha na kubadilisha jamii uliofanyika jijini Dar es Salaam,Richmond alisema kuwa tatizo la  kuondokana na umaskini halihusu serikali peke yake bali linahusu sekta zote zikiwemo  zisizo za kiserikali ambazo zinajumuisha viwanda na makampuni mbalimbali yanayofanya biashara nchini.
Mhandisi Richmond alitoa mfano wa kampuni ya TBL Group ambayo ni mwajiri wake kuwa imeweka mifumo na miongozo inayoelekeza kuipa kipaumbele miradi ya kijamii na alidai kuwa tayari imeanza kuleta mabadiliko chanya na kubadilisha maisha ya watanzania wengi.
 
Aliitaja baadhi ya miradi ambayo imeonyesha mafanikio kuwa ni mradi wa kilimo shirikishi wa Go farming ambao kampuni inawasaidia wakulima kwa kuwapatia pembejeo,utaalamu na kuhakikishia uhakika wa soko la mazao yao ,mradi ambao umewanufaisha wakulima wa zao la Shahiri kwenye mikoa ya kanda ya Kaskazini mwa Tanzania na kuongeza ajira ya wafanyakazi wa mashambani ambao alidai utaanza kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini.
Miradi mingine aliitaja kuwa ni kusaidia miradi ya maji,kusaidia miradi ya Afya hususani ya kupambana na ugonjwa wa Malaria,kuwezesha akina mama wanaouza pembe ya chibuku kupitia vikundi vinavyojulikana kama Chibuku Mamas,kutoa elimu ya biashara kwa wafanyabiashara wadogowadogo wanaoendesha biashara ya vinywaji , kusaidia kutoa elimu ya Usalama barabarani na kuhamasisa wafanyakazi wake kutenga muda wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii.
Pia Richmond alisema kuwa kampuni imeanza kutumia teknolojia za kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kutumia mtambo wa uzalishaji usiotumia nishati ya mafuta kama ilivyozeleka katika uzalishaji wa viwandani bali inatumia pumba za mpunga.
“Teknolojia hii ya aina yake barani Afrika ambayo imeanza kutumika kwenye kiwanda cha TBL Mwanza ninachokiongoza ni muhimu kuanzishwa katika viwanda mbalimbali kwa kuwa inasaidia katika  utunzaji wa mazingira”.Alisema.

Aliongeza kuwa mbali na kutunza mazingira imewezesha wakulima wa zao la mpunga kunufaika kwa kuuza pumba za mpunga ambazo zamani zilikuwa zinatupwa sasa ni malighafi kubwa ambayo imeanza kubadilisha uchumi wa wananchi “Huu ndio uwekezaji wenye ubunifu unaobadilisha maisha ya wananchi na kutoa mchango katika kupunguza umaskini nchini”Alisema

Related

Biashara 3390265520594375944

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item