Mourinho huyo kuifundisha Man U msimu ujao. | LUKAZA BLOG

Mourinho huyo kuifundisha Man U msimu ujao.

Hatimaye tetesi zinageuka kuwa kweli, Manchester United watamtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao, shirika la utangazaji la Uingereza BBC...

Hatimaye tetesi zinageuka kuwa kweli, Manchester United watamtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao, shirika la utangazaji la Uingereza BBC limeripoti.

 Mourinho amekuwa nje ya kazi tangu alipofukuzwa kazi na Chelsea mnamo December 2015. 
Huku United wakiwa wameshindwa kufuzu kucheza Champions League chini ya Louis van Gaal – viongozi wa Old Trafford wameamua kufanya mabadiliko. 
Inaeleweka dili na kocha huyo mwenye miaka 53 lilifanyika kabla ya mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace.
United wanategemewa kumtangaza rasmi Mourinho mapema wiki ijayo baada ya kumtaarifu Van Gaal kuhusu mwisho wa ajira yake. 
Van Gaal bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa miaka 3, lakini pamoja na kutumia £250m utawala wake umekuwa wa majuto kwa klabu na kuwaacha mashabiki wengi wakiwa hawaridhiki na utendaji wake, msimu wa kwanza alimaliza nafasi ya 4, na msimu huu watano.  
 Mourinho ni mmoja wa makocha bora katika ulimwengu wa soka, akishinda makombe matatu ya ligi katika vipindi viwili vya kazi ndani ya Chelsea, pamoja kuziongoza Porto na Inter Milan kutwaa Champions League – pia akibeba ubingwa wa La Liga na RealMadrid

Related

Michezo 4399788468185675656

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item