Ndege Kubwa kuliko zote duniani aina ya Antonov An-225 yatua nchini Australia | LUKAZA BLOG

Ndege Kubwa kuliko zote duniani aina ya Antonov An-225 yatua nchini Australia

 Ndege aina ya  Antonov An-225 ambayo iliwahi kutua Jijini Dar Es Salaam Mwaka 2006 ikiwa inasafirisha majenereta imetua kwa mara ya kwan...

 Ndege aina ya Antonov An-225 ambayo iliwahi kutua Jijini Dar Es Salaam Mwaka 2006 ikiwa inasafirisha majenereta imetua kwa mara ya kwanza nchini Australia 
 Mikia Pacha ya Ndege aina ya Antonov An-225
Matairi ya ndege aina ya Antonov An-225
Ndege aina ya Antonov An-225 Mriya ambayo ni kubwa kuliko zote duniani kwa mara ya kwanza imetua katika ardhi ya nchi ya Australia ambapo mamia ya wakazi wa nchi hiyo walijitokeza kushuhudia ndege wakati ilipokuwa ikisafirisha jenereta lenye uzito wa tani 117 . Ndege Antonov An-225 Mriya ni ndege inayobeba mizigo huku ikiwa na urefu wa mita 84 na uzito wa tani 175 ikiwa haijabeba kitu chochote ndani yake. 
Ndege hiyo ya Antonov An-225 Mriya iliwasili mjini Perth nchini Australia ikitokea mjini Prague na kusimama maeneo kadhaa ya MAshariki ya Kati na Asia kabla ya kutua nchini Australia
Ikumbukwe kuwa Ndege hiyo aina ya Antonov An-225 Mriya ilimeshatua katika viwanja mbalimbali vya ndege duniani na Tanzania ikiwepo
Ndege hiyo aina ya Antonov An-225 Mriya ilitua katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwl Julius Kambarage Nyerere mnamo Oktoba, 30 2006
Ndege hiyo aina Antonov An-225 inz Matairi manne mbele huku nyuma ikiwa na matairi 28 ambapo hufanya jumla ya matairi 32 katika ndege hiyo. Ina mkia pacha tofauti na ndege nyingine nyingi za kubeba abiria na mizigo. Huku ikiwa na injini sita aina ya Jet

Related

Makala 5301688276114019229

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item