Chadema yafungu kesi mahakama kuu kanda ya Mwanza dhidi ya polisi | LUKAZA BLOG

Chadema yafungu kesi mahakama kuu kanda ya Mwanza dhidi ya polisi

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kan...

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini.

Kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, ilifunguliwa jana na kusimamiwa na
mawakili watatu Gasper Mwanalyela, John Mallya na Paul Kipeja.
 
Licha ya kuwepo na ulinzi mkali wa jeshi la polisi uliowekwa katika barabara  zote za kuelekea Mahakama Kuu, viongozi na wafuasi wa Chedema  walifanikiwa kuvuka vizuizi hivyo.
 
Akizungumza na waandishi wa  habari baada ya kutoka mahakamani jana jioni, Mbowe alisema sababu za  kufunguliwa kwa kesi hiyo ni baada ya kuona demokrasia ya vyama vingi "inabakwa nchini."Mbowe alisema watu wanne waliotajwa katika kesi hiyo ya madai ni Kamanda wa Polisi wilayani Geita, Kamanda wa Polisi  wilayani Kahama, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa polisi (Makao  Makuu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Alisema wadaiwa hao  wamefunguliwa kesi kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa nchini kwa kuchukua maamuzi ambayo hayaendani na demokrasia.
 
“Tunaiomba  mahakama itangaze amri ya jeshi la polisi ya kuzuia mikutano ya vyama  vya siasa ni batili, utekelezaji unaofanywa ni batili, polisi wapewe
tangazo la kutowanyanyasa wapinzani na pia itoe amri ya vyama vya siasa
kufanya mikutano yake na polisi wawe walinzi wa mikutano hiyo,” alisema
Mbowe.
 
Alisema pamoja na polisi kuwabana hawataondoka jijini Mwanza, na wataongezeka zaidi mpaka kieleweke.
 
Alisema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha Chadema inafutika katika mikoa ya  Kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya viongozi wake kutekwa na kunyanyaswa na polisi.
 
Mkutano huo na waandishi wa habari ulihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Issa Mohamed, Dk. Vincent Mashinji  (Katibu Mkuu), Salum Mwalimu (Naibu Katibu Zanzibar), Halima Mdee  (Mwenyekiti Bawacha) na Pastrobass Katambi (Mwenyekiti Bavicha) na  baadhi ya wabunge wa chama hicho.
 
Kesi hiyo ya madai inatarajiwa kupangiwa Jaji Jumatatu ijayo.
 
Polisi ilisambaratisha mkutano wa Chadema uliokuwa ufanyike Kahama katikati ya wiki, ambapo mabomu ya machozi na magari ya 'washawasha' vilitumika  kuondoa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wasikilize hotuba za viongozi  wa kitaifa.
 
Chadema imepanga kufanya mikutano nchi nzima kulaani inachodai uonevu unaofanywa dhidi ya wabunge wake Bungeni.

Related

Siasa 7712071961603171304

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item