Jumia Tanzania wahamishia huduma zao zote katika tovuti Moja | LUKAZA BLOG

Jumia Tanzania wahamishia huduma zao zote katika tovuti Moja

Mkurugenzi mtendaji wa Jumia House, Jumia Deals pamoja na Jumia Jobs, Ndg Pierre Francois akielezea mbele ya waandishi wa habari kuhusian...

Mkurugenzi mtendaji wa Jumia House, Jumia Deals pamoja na Jumia Jobs, Ndg Pierre Francois akielezea mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na Mpango wa huduma zote za Jumia kuwekwa sehemu kwaajili ya kuwarahisishia wateja wao kupata huduma zote sehemu, mfumo huo unaitwa Jumia Ecosystem ambao humuwezesha mtembeleaji wa tovuti kupata huduma zote za jumia katika tovuti moja.
Laurtiz Elmshauser , Mkurugenzi Mkazi wa Jumia akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jana katika ukumbi wa Buni uliopo Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam katika Jengo la COstech ambapo mkurugenzi huyo alisema wameamua kufanya hivyo kwaajili ya kuwarahisishia wateja wao kupata huduma zote katika tovuti moja ambapo mfumo huo uitwa Jumia Ecosystem.
 Nina Holmes Mkurugenzi mtendaji wa Jumia Tanzania akielezea juu ya brands zote za jumia kuingia katika mfumo mmoja uitwao Jumia Ecosystem ambao utamwezesha mtembeleaji au mteja wa jumia kupata huduma zote mahali pamoja ambapo sasa imekuwa rahisi kwa wateja wao kuweza kupata huduma kirahisi tofauti na mwanzo ambapo kila brands au huduma ya jumia ilikua na tovuti yake. Kwa sasa unaweza kupata huduma za jumia kupitia Mfumo wao mpya ujulikanao kama Jumia Ecosystem kwa kutembela tovuti yao ya https://www.jumia.co.tz na kuweza kuchagua huduma unayoitaka ambapo kuna huduma za kununua magari, nguo, Chakula, Kukata tiketi, na tovuti ya ajira.
 Nina Holmes Mkurugenzi mtendaji wa Jumia Tanzania akitoa maelezo mbele ya waandishi wa habari jana wakati akizungumzia jinsi walivyoweza kuhamisha huduma zao katika mfumo wa Jumia Ecosystem ambapo huduma zote za jumai zinapatika mahala pamoja kupitia tovuti ya www.jumia.co.tz
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini
Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Lilian Kisasa akitoa Utambulisho kwa waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo kwaajili ya kutambulisha jinsi Jumia Tanzania ambavyo wanaendelea kutoa mazingira rafiki kwa wateja wao.
 Mkurugenzi mtendaji wa Jumia House, Jumia Deals pamoja na Jumia Jobs, Ndg Pierre Francois akijibu baadhi ya maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Buni uliopo katika Jengo la Costech Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Related

Hot Stories 5579581736420387003

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item