KAMATI YA MAWASILIANO MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO. | LUKAZA BLOG

KAMATI YA MAWASILIANO MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Mkoa wa Mwanza, Jonathan Abdallah Kasibu, akizungumza katika Semina kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasi...

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Mkoa wa Mwanza, Jonathan Abdallah Kasibu, akizungumza katika Semina kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanza.

Katika semina hiyo, watumiaji wa hudumza za mawasiliano ikiwemo simu pamoja na vyombo vya habari ambao waliwakilisha makundi mbalimbali kama vile wanahabari, wajasiriamali na

walemavu, walipewa elimu juu ya uwepo wa Kamati hiyo pamoja na uwepo wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC).

Pia walielimishwa juu ya mwongozo wa kuwasilisha malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za

Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC) ambapo iliambatana na viongozi wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza kujitambulisha kwa baraza  hilo.

Watumiaji wa huduma za mawasiliano walielezwa kwamba ni wajibu wao kuwasilisha malalamiko yao ikiwa wanapokea huduma zilizo chini ya kiwango ama ikiwa wana malalamiko ya aina yoyote kuhusu huduma za mawasiliano.

Walihimizwa kuwasilisha malalamiko yao kwa kuanza na mtoa huduma, yasiposhughulikiwa wanawayawasilisha katika Kamati ya Huduma za Mawasiliano mkoa, yasipotatuliwa yatawasilishwa katika  Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka TCRA na hata

ngazi nyingine zaidi hadi pale utatuzi utakapofanyika.

Semina hiyo ilionekana kuwafungua ufahamu watumiaji wa huduma za mawasiliano jijini Mwanza kwani baadhi yao walieleza kuwa awali walikuwa hawatambui haki na wajibu wao katika

kutumia huduma za mawasiliano.
Baadhi ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza, wakiwa katika semina ya kuwaelimisha juu ya Matumizi ya Huduma za Mawasiliano.

Related

kitaifa 7774498014362727967

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item