Kampeni ya Media Car Wash for Health yafana mjini Dodoma | LUKAZA BLOG

Kampeni ya Media Car Wash for Health yafana mjini Dodoma

    Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo.   Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ak...

   Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo. Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiosha gari la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota wakati wa kampeni ya Media Car Wash ya kuchangisha fedha za kusaidia wanahabari kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti  na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani  wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya  Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa
habari nchini. 

Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalimbali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza  kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari  ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.  Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani.
 
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) wakishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya  kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari  ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 

Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo.

Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na mpiga picha wa magazeti ya The Guardian Ltd, Halima Kambi wakiosha moja ya gari katika kampeni hizo. 

Related

Kijamii 291453842270430653

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item