Kesi ya Kizza Besigye yaahirishwa tena | LUKAZA BLOG

Kesi ya Kizza Besigye yaahirishwa tena

Image copyright AP Image caption Kesi ya Kizza Besigye yaahirishwa tena Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kizza Besigye aliyekuwa ana...

Image copyrightAP
Image captionKesi ya Kizza Besigye yaahirishwa tena
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kizza Besigye aliyekuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu shtaka la uhaini hajafikishwa mahakamani.
Upande wa mashtaka umeomba ruhusa mahakama hiyo ihamishwe karibu na gereza alikozuiliwa bw Besigye kwa ajili ya tishio la amani mjini.
Hata hivyo viongozi wengine wa upinzani wamejaa mahakamani ambapo wanafanya mgomo baridi.
  • Besigye ashtakiwa kosa la uhaini Uganda
  • Besigye ahamishiwa gereza la Kampala
  • B esigye akamatwa kwa 'kujiapisha' Uganda
Hakimu aliyekuwa anatarajiwa kusikiza kesi hiyo aliagiza kuahirishwa kwa kusikizwa kwa kesi hiyo hadi tarehe 15 mwezi huu wa sita.
Bw Besigye ndiye aliyekuwa mshindani wa karibu wa Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa February 2016.
Kiongozi huyo wa upinzani anadai kuwa alishinda katika uchaguzi huo, ambao ulikosolewa na wangalizi wa kimataifa.
Image copyrightREUTERS
Image captionBw Besigye ndiye aliyekuwa mshindani wa karibu wa Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa February 2016.
Hatua yake ya kujiapisha kuwa rais ndiyo iliyomkasirisha rais Museveni ambaye ndiye ameanza hatamu yake ya tano uongozini na kusababishwa kukamatwa kwake kwa kukiuka katiba kwa kosa la uhaini.
Besigye amekuwa akishikiliwa na polisi kwa muda wa siku kumi na mbili baada ya mahakama huko Moroto kuagiza awekwe rumande hadi Juni mosi.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.Chanzo BBC Swahili

Related

Kimataifa 330099860852399743

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item