King'ora cha gari la Mitsubishi Outlander chadukuliwa | LUKAZA BLOG

King'ora cha gari la Mitsubishi Outlander chadukuliwa

Image copyright AFP Image caption Mistubishi Outlander King'ora cha gari aina ya Mitsubishi Outlander kinaweza kuzimwa kupitia wi-fi ...

Image copyrightAFP
Image captionMistubishi Outlander
King'ora cha gari aina ya Mitsubishi Outlander kinaweza kuzimwa kupitia wi-fi yake iliopo ndani,watafiti wamebaini.
Mwanya huo unamaanisha kwamba wezi wanaweza kuingia na kutumia tatizo hilo la usalama wa gari hilo kupata mda wa kuvunja,kuingia na kuliiba gari hilo.
Vilevile mwanya huo unaweza kutumika kufanyia udanganyifu mazingira ya gari hilo na kumaliza nguvu betri yake.
Mitsubishi imewataka watumizi wa magari hayo kuzima mtandao wa gari hilo huku ikiendelea kuchunguza tatizo hilo na mfumo wa gari hilo.
Image copyrightMITSUBISHI
Image captionMitubishi Outlander Hybrid
Mtaalam wa maswala ya kiusalama Ken Munro anasema kuwa uchunguzi ulianza wakati alipokuwa akingojea kuchukua watoto wake kutoka shule na kubaini uingiliaji wa mtandao wa gari hilo katika orodha ya simu yake.
Baadaye alibaini kwamba ni gari la Mitsubishi Outlander ambalo ni la rafikiye ambaye aliomuonyesha programu hiyo na vile inavyoweza kutumika kudhibiti gari hilo.

Related

Kimataifa 7847182485411603968

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item