MAREKANI YAICHAPA PARAGUAY 1-0 NA KUONGOZA KUNDI LAO, COLOMBIA YALALA 3-2 KWA COSTA RICA | LUKAZA BLOG

MAREKANI YAICHAPA PARAGUAY 1-0 NA KUONGOZA KUNDI LAO, COLOMBIA YALALA 3-2 KWA COSTA RICA

Na Dac Popos, Globu ya Jamii. Marekani imefanikiwa kuongoza kundi A mara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Paraguay. Ikic...

Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

Marekani imefanikiwa kuongoza kundi A mara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Paraguay. Ikicheza mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wake kwenye uwanja wa Lincoin Financial Field jijini Philadelphia, Marekani ilionyesha kiwango kizuri cha uchezaji na kunako dakika ya 27 Clint Dempsey aliifungia Marekani bao hilo pekee katika mtanange huo.

Ingawa Marekani walicheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa muda mrefu wa mchezo, kwani dakika ya 36 beki wa kulia wa Marekani Yedlin alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano, bado Marekani waliweza kulilinda lango lao na kushambulia kwa kushitukiza. Hadi mwisho Marekani 1, Paraguay 0.

Kwa kuongoza kundi kuna uwezekano mkubwa kuwa Marekani akawa amekwepa kukutana na Brazil katika hatua ya mtoano.
Kwenye mchezo kati ya Colombia na Costa Rica, kocha Jose Pekerman wa Colombia aliwapanga nyota wake kama wachezaji wa akiba kitu ambacho alikijutia baadaye, baada ya timu yake kupata kichapo cha mabao 3-2 toka kwa Cost Rica. 

Kituko au kivutio kwenye mchezo huu ilikuwa kwa mchezaji wa Colombia Frank Fabra, yeye alifunga mabao mawili, moja kwa kila timu yaani aliifungia timu yake dakika ya 7 na akaifungia timu pinzani (Costa Rica) dakika ya 34.

Mabao mengine ya Costa Rica yalifungwa na Johan Venegas dakika ya 2 na Celso Borges dakika ya 58. Na lingine la Colombia lilifungwa na Marlos Moreno.

Leo tutawashuhudia
HAITI vs EQUADOR
BRAZIL vs PERU

Related

Michezo 973038083888777656

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item