Proinbox suluhisho la wateja wa filamu nchini Tanzania. | LUKAZA BLOG

Proinbox suluhisho la wateja wa filamu nchini Tanzania.

Tasnia ya filamu nchini Tanzania imeendelea kukua, huku teknolojia ikiwa ndio sababu kubwa haswa ya kufanya kila kitu kiendane na kasi ya...

Tasnia ya filamu nchini Tanzania imeendelea kukua, huku teknolojia ikiwa ndio sababu kubwa haswa ya kufanya kila kitu kiendane na kasi ya ukuaji wa tasnia hiyo. Teknolojia inapokwenda kwa kasi hupelekea watu binafsi, taasisi na hata makampuni kuendana na kasi hiyo ili kusudi wasiachwe nyuma na teknolojia huku dunia ikiendelea kwa kasi kutokana na wadau kujaribu kuendana na kasi hiyo.

Katika kuendana na kasi ya teknolojia nchini Tanzania katika sekta ya filamu, Kampuni ya Proin Promotions ndio imekuwa kampuni ya kwanza nchini Tanzania kuhakikisha inawafikia wateja wengi zaidi duniani kote kutokana na kukimbizana sambamba na ukuaji wa teknolojia katika kuhakikisha inawafikia wapenzi wa filamu hususani waliopo nje ya nchi na wanapenda filamu za Tanzania.

Kwa mara ya kwanza Kampuni ya proin promotions ilizindua mfumo wa kuuza filamu zake kupitia mtandao ambapo takribani ya wakazi wapatao elfu moja walipata uwezo wa kununua filamu tofauti tofauti kupitia mtando ndani ya mwezi mmoja tokea kuanzishwa kwake.Mfumo huo uliwasaidia sana Watanzania wengi waishio nje ya nchi kuweza kununua filamu za kitanzania kwa bei nafuu huku wakiweza kutazama kupitia tv zao bila kuhangaika kutumiwa kutoka nchini Tanzania. Unaweza kununua filamu za kitanzania kupitia mtandao wao wa http://www.proinpromotions.co.tz.
Wiki chache zilizopita kampuni hiyo hiyo ya Proin Promotions imeweza kuwafikia watanzania wengi zaidi na zaidi na kuwaondolea usumbufu wa kwenda kwenye maduka ya kuuzia filamu kwa kuwaletea application inayoitwa PROINBOX ,application hii inapatika katika mfumo wa uendeshaji wa Android katika ghala ya android ijulikanayo kama google play. Application hii inampa uwezo mtumiaji yoyote yule wa simu yenye mfumo wa uendeshaji wa android kuweza kununua filamu ya Kitanzania na kuiangalia kupitia simu yake ya mkononi mahala popote pale alipo na kuweza kulipia hapo hapo kupitia simu yake ya mkononi bila kwenda mahali popote pale. Application hii imeweza kuleta mabadiliko ya hali ya juu sana katika tasnia ya filamu ambapo sasa watu wengi waliokuwa wamekosa muda na nafasi ya kwenda kwenye maduka ya kununulia filamu basi sasa wanaweza kununua filamu kupitia simu zao za mkononi huku ubora wa filamu huo ukiwa sawasawa na ule ambao angeupata katika mfumo wa DVDs, Mfumo huu wa PROINBOX ni mfumo salama na wa uhakika kutokana na jinsi ulivyoweza kutengenezwa kwaajili ya kutimiza mahitaji ya wapenzi wa filamu nchini. 

Ili kuweza kununua filamu za kitanzania kupitia application hii ya PROINBOX unachotakiwa kufanya kwanza ni kupakua (download) app ya proinbox kupitia google play na sanikisha katika simu yako (Install) baada ya hapo unatakiwa kujisajili kwa kutumia namba yako ya simu ya mtandao wowote ule ambapo utaweza kuingia (log in) na kuanza kufurahia huduma na sinema zetu, Pia unaweza kuangalia filamu za Mpango Mbaya na nyingine bure kupitia app hii ya proinbox

Mnamo tarehe 15 July 2016 Proin promotions ltd wataizindua rasmi application hii huku ikienda sambamba na uzinduzi wa filamu ya Ni Noma iliyochezwa na Mshindi wa Tuzo ya filamu bora ya Afrika Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu. Filamu hiyo pia itaweza kuuzwa kupitia PROINBOX na kwa bei nafuu kabisa kwa wale wapenzi na mashabiki wa filamu za kitanzania wanaomba kusanikisha (install) application hii ya proinbox kwaajili ya kuhakikisha kila movie mpya inayotoka basi wanaweza kuipata na kununua kupitia simu zao za mkononi.

Kama hujafanikiwa kuwa na app hiyo katika simu yako basi fuata link hii kwaajili ya kuhifadhi kwenye simu yako bofya PROINBOX au http://proinbox.co.tz/

Related

Makala 3700122891715767352

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item