Rais Magufuli - Najua wewe ni mtangazaji Mzuri ufanye kama unatangaza tangaza tu Maendeleo huko unapokwenda | LUKAZA BLOG

Rais Magufuli - Najua wewe ni mtangazaji Mzuri ufanye kama unatangaza tangaza tu Maendeleo huko unapokwenda

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amewaapisha wakuu wapya wa wilaya 139 na wakuu wa mikoa wanne kwenye hafla iliyofanyika ikulu jijini Da...

Rais Dkt John Pombe Magufuli leo amewaapisha wakuu wapya wa wilaya 139 na wakuu wa mikoa wanne kwenye hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli akiwa na baadhi ya wakuu wa wilaya kwenye picha ya pamoja Ikulu Jumatano hii

Miongoni mwa wakuu wa wilaya wapya ni mtangazaji nguli wa redio na TV, Godwin Gondwe. Gongwe sasa ni mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Akiongea kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli anayefahamika kwa utani mwingine alimsifia Gondwe kuwa ni mtangazaji mzuri na kumtaka atumie uwezo huo kutangaza maendeleo.

“Gondwe najua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu,” alisema.

Godwin Gondwe kama anavyojulikana pia alikuwa mtangazaji maarufu wa habari kwenye kituo cha runinga cha ITV. Amewahi pia kufanya kazi kwenye vituo vya redio vya Radio Free Africa na Radio One. Lakini pia alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam.

Related

Hot Stories 8988608951812846655

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item