SANAA JWTZ YAKONGA NYOYO ZA WANANCHI DODOMA | LUKAZA BLOG

SANAA JWTZ YAKONGA NYOYO ZA WANANCHI DODOMA

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jamine Tisekwa akiungana na kwaya ya Kikundi cha Sanaa za Maonesho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ...

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jamine Tisekwa akiungana na kwaya ya Kikundi cha Sanaa za Maonesho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati burudani ikitolewa bure kwa wananchi katika Bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Sanaa JWTZ ilitoa pia burudani za sarakasi, taarabu, ngoma za asili, Steel Band na muziki wa bendi ya Mwenge Wana Paselepa

Burudani hiyo ilikonga nyoyo za  wananchi waliofurika kushuhudia ambapo hata muda wa kumaliza ulipowadia hawakutaka watoke eneo hilo.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya kuhusu onesho hilo, alisema kuwa ni jambo ambalo hawakulitegemea hivyo wanaomba tena Sanaa JWTZ wapange siku nyingine waburudishe kuanzia mapema saa nane  hadi jioni ili wananchi wa mkoa huo wafarijike vya kutosha.

Baada ya kumalizi hapo kundi hilo la Sanaa Jwtz lilikwenda kutumbiza usiki kwenye Chuo cha Mipango Dodoma.

Akizungumza Msemaji wa JWTZ SANAA, Hope Dagaa alisema hivi sasa kikundi chao wamekiboresha na kwamba hivi sasa wanataka warudi kwa nguvu zote kwenye kumbi kutoa burudani murwa kwa wananchi, kama ilivyo kuwa zamani. HABARI,PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkuu wa Wilaya akicheza pia ngoma ya kibati ya asili ya Zanzibar
 Ngoma ya kibati
 Mwenge Jazz ikifanya vitu vyake
 Wananchi wakishuhudia

 Steel Band ikitumbuiza

 Umati wa wananchi wa Dodoma wakifarijika na burudani murwa iliyokuwa ikitolewa hapo

 Ngoma ya kibati ikichukua nafasi yake Mkuu wa Wilaya akiwatuza wasanii

 Msemaji wa Sanaa JWTZ, Hope Dagaa akiwa na Mkuu wa Wilaya Tisekwa

 Mkuu wa Wilaya akicheza wakati kwaya ikitumbuiza Mkuu wa Wilaya, Tisekwa akiwa na wasanii wa JWTZ

 Kikundi cha Kwaya

 Steel Band

 Band ya Mwenge Jazz
Taarab na Sarakasi

Related

Burudani 8612201584620850359

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item