Serikali yapiga marufuku uagizaji wa transfoma za umeme kutoka nje ya nchi. | LUKAZA BLOG

Serikali yapiga marufuku uagizaji wa transfoma za umeme kutoka nje ya nchi.

Jonas Kamaleki-Maelezo Serikali imeliagiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kutoagiza  transfoma nje ya nchi na badala yake ...


Jonas Kamaleki-Maelezo

Serikali imeliagiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kutoagiza  transfoma nje ya nchi na badala yake kutumia zinazotengenezwa hapa  nchini na kampuni ya Tanalec.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni  Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani  alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Mhe. Daimu Iddi  Mpakate aliyetaka kujua ni lini Serikali itatoa pesa kukamilisha miradi ya umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Dkt. Kalemani  alisema uzalishaji wa transforma ni mkubwa ikilinganishwa na mahitaji ya bidhaa hizo kwa mwezi, hivyo hakuna sababu ya kuagiza transforma hizo  kwa bei kubwa wakati zinapatikana hapa nchini.

Kuhusu suala la  kugharamia nguzo kwa Mpango wa REA Dkt. Kalemani alisema mteja hatakiwi  kutozwa gharama yoyote ziadi ya Tshs. 27,000 fedha ya kuunganishiwa  umeme kwa mpango huu.Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali inatekeleza  Mradi wa REA Awamu ya II katika Wilaya ya Tunduru na kazi hii  inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2016.

Alisema  Kazi ya kupeleka umeme katika wilaya hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa Kilomita 293. 2, na ujenzi  wa njia nyingine yenye msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita  76.1 na ufungaji wa transfoma 38 pamoja na kuwaunganishia umeme wateja  wa awali 3,330

“Gharama ya Mradi kwa Mkoa wa Ruvuma ikiwemo  Wilaya ya Tunduru ni Tsh. Bilioni 32.56,” alisema Dkt Kalemani na  kuongeza kuwa mkandarasi amekwishalipwa bilioni 27.22 sawa na asilimia  83.6 ya fedha.  Dkt. Kalemani amesema kuwa katika Wilaya ya Tunduru  ni vijiji vinne ambavyo vimeunganishiwa miundombinu ya umeme na  kufanyiwa majaribio kabla ya kuwashiwa umeme.

Kwa mujibu wa  Dkt. Kalemani mkandarasi anaendelea kufunga transforma na Mita za Luku  katika vijiji 34 vilivyosalia kwa Wilaya ya Tunduru ili viweze kupatiwa  huduma ya umeme ifikapo tarehe 30 Juni, 2016.

Related

Hot Stories 6938589580414482483

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item