Siku China Wakichukua Kombe La Dunia Usishangae. Sababu Ni Kama Hii Hapa | LUKAZA BLOG

Siku China Wakichukua Kombe La Dunia Usishangae. Sababu Ni Kama Hii Hapa

Evergrande Football School-China   Na BongoCelebrity.Com China ni nchi ambayo inajengwa kwa dhamira. Wakidhamiria kufanya kitu fula...

Evergrande Football School-China
 
Na BongoCelebrity.Com

China
ni nchi ambayo inajengwa kwa dhamira. Wakidhamiria kufanya kitu fulani,
watafanya kila linalowezekana kufanikisha. Ni miongoni mwa mataifa ya
watendaji. Wanaongea lakini huku wanaongea,wanatenda. Waliwahi
kudhamiria kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu ya kiuchumi dunia. Leo  sote tunajua wapo wapi.

Hivi sasa China wamedhamiria kuja  kuchukua ubingwa wa soka duniani kwa maana ya Kombe la Dunia la Soka  (Soccer World Cup). Ni dhamira na dira ambayo inaungwa mkono na Rais wao Xi Jinping ambaye ni mpenzi wa mpira toka utotoni.

Zipo nukuu ambazo zinasema Rais Xi Jinping aliwahi kusema mojawapo ya ndoto zake kuu ni kuona China ikiwa mwenyeji wa Kombe la Dunia na hatimaye kushinda kombe hilo. Mpaka hii  leo China iliwahi kushiriki katika fainali za Kombe La Dunia mara moja  tu. Ilifanya hivyo mwaka 2002 wakati michuano hiyo ilipofanyikia Korea  Kusini na Japan. China walitoka kapa bila kufunga hata goli moja.

Miaka miwili iliyopita serikali ya China ilitangaza kwamba soka ni sehemu ya  mitaala mashuleni. Hivi sasa wapo katika programu za kujenga viwanja na programu za mafunzo ya soka katika shule zaidi ya elfu ishirini
(20,000). Miradi na programu hizo zinalenga katika kuibua wachezaji
wapya wa soka zaidi ya 100,000 na ambao watajikita katika kuiletea China
hiyo heshima inayoisaka.

Mbali ya programu hiyo ya kiserikali na bila shaka kwa shule za serikali, zipo shule binafsi ambazo zinaelekea  kufuata mkondo huo. Mojawapo ni Evergrande Football School(sisi  tunaziita hizi Academy). Shule hii iliyopo Qingyuan, Guangdong,China  (Kusini mwa China) ndio Football Academy kubwa kuliko zote ulimwenguni.  Ilifunguliwa rasmi mwaka 2012.
Shule ya Evergrande Football School inavyoonekana kwa juu. Ina ukubwa wa ekari zaidi ya 300

Inamilikiwa na kampuni ya Evergrande Group ambayo ni ya bilionea Xu Jiayin ambaye pia anamiliki timu ya Guangzhou Evergrande Football Club.Ni
shule ya boarding ya primary na sekondari (full-time boarding primary
and secondary football school). Wanafanya mazoezi siku 6 kwa wiki.

Related

Michezo 218228318743284915

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item