SIMU FEKI KUZIMWA RASMI KESHO - TCRA | LUKAZA BLOG

SIMU FEKI KUZIMWA RASMI KESHO - TCRA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es S...

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuzima simu feki ifikapo kesho Juni 16 mwaka huu.
Meneja wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila kibuda, Globu ya Jamii.
SIMU zilizoingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi kesho, katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu kiwango kwa usalama  na ulinzi wa nchi.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.
Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa kutokana na kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10.

Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu wajiandae zoezi hilo na simu zitazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika mazingira salama.

Aidha amesema katika elimu wametoa hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.

‘’Simu feki kesho kuzimwa. Hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu simu ya  feki ambazo baada soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba  .

Related

Hot Stories 6171231605921929575

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item