Sterling Pound yaporomoka kiwango kikubwa zaidi | LUKAZA BLOG

Sterling Pound yaporomoka kiwango kikubwa zaidi

Image caption Sterling Pound yaporomoka kiwango kikubwa zaidi katika miaka 30 Thamani ya sarafu ya Uingereza, Sterling pound imeshuka kwa...

Image captionSterling Pound yaporomoka kiwango kikubwa zaidi katika miaka 30
Thamani ya sarafu ya Uingereza, Sterling pound imeshuka kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.
Wafanyibiashara wamepandwa na ghadhabu kubwa kutokana na matokeo ya kura ya maoni nchini Uingereza ambayo imeonesha wazi kuwa asilimia 52% ya Waingereza wangependa taifa hilo lijiondoe katika muungano wa EU.
Katika saa ya kwanza ya kuhesabu kura hiyo ya maoni, pauni ya Uingereza ilipanda na kuishinda dola ya Marekani, lakini kwa sasa imeshuka baada ya matokeo ya kura hiyo kuanza kuonyesha dalili ya Uingereza kujiondoa kutoka katika muungano wa mataifa ya bara Ulaya.
Wafanyibiashara wanasema kuwa hawajawahi kushuhudia mabadiliko makubwa ya kifedha kiasi hicho tangu wakati wa mdororo wa uchumi mwaka 2008.
Image copyrightAP
Image captionGavana wa benki kuu ya Uingereza kutoa mwelekeo kuhusiana na hatma hiyo
Masoko ya hisa katika mataifa ya bara Asia yameshuhudia pia mdororo kama huo huku Yen ya Japan ikishuka kwa thamani kubwa pia.
Thamani ya soko la hisa la Japan tayari limeshuka kwa asilimia 8.
Taasisi inayoratibu ubora wa soko na chumi wa mataifa mataifa Standard and Poor imeonya kuwa sasa Uingereza huenda ikapoteza ubora hadhi yake ya kuwa soko lenye uthabiti kuliko yote duniani ama 'triple A rating'
Wadadisi wa maswala ya kiuchumi wanatabiri kuwa soko la hisa la Uingereza mjini London pia litaporomoka kufuatia kauli hiyo ya waingereza.
Gavana wa benki kuu ya Uingereza anatarajiwa kutoa mwelekeo muda mchache ujao kuhusiana na hali ya kiuchumi na sarafu ya Uingereza Sterling pound, katika muda mchache ujao.

Related

Kimataifa 8419208912849021800

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item