TUNDU LISSU AWEKWA RUMANDE KWA KUKOSA DHAMANA. | LUKAZA BLOG

TUNDU LISSU AWEKWA RUMANDE KWA KUKOSA DHAMANA.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la P...

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa si ya kiungwana.

Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa  Mbunge Lissu kuripoti  katika kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi hilo kuhusu kauli yake aliyoitoa jana baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu  kuhusiana na maneno mengine ambayo anayodaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekili kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.

Related

Siasa 6906155808601505279

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item