Wafanyakazi TBL washiriki kuishangilia Taifa Stars | LUKAZA BLOG

Wafanyakazi TBL washiriki kuishangilia Taifa Stars

Kundi la washabiki wakishangilia  kwa mbwembwe wakati wa mchezo huo Licha ya Taifa Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya timu ya ...


Kundi la washabiki wakishangilia  kwa mbwembwe wakati wa mchezo huo

Licha ya Taifa Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya timu ya Taifa ya Misri watanzania wengi walikuwa wamejitoa kwa kila hali kuishangilia katika mchezo huu wa nyumbani uliokuwa unafuatiliwa kwa karibu na wapenzi wa soka nchini kote.
Katika kuhakikisha wachezaji wa Taifa Stars wanaongezewa hamasa ya kucheza kwa kushangiliwa, kampuni ya TBL Group ambayo ni mmoja wa wadhamini wa timu ya taifa mwishoni mwa wiki iliwawezesha  baadhi ya wafanyakazi wake ,familia zao na baadhi ya mawakala wa kuuza bidhaa zake kuangalia mpambano wa Taifa Stars na timu ya taifa ya Misri.
Lengo kubwa la kuwapatia tiketi za mchezo wafanyakazi wake na baadhi ya wateja lilikuwa ni kuiongezea nguvu Taifa Stars kwa kuishangilia.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na msisimko mkubwa na kuwavutia maelfu ya washabiki wa soka nchini Taifa Stars ilifungwa mabao 2-0 na timu ya Misri ‘The Pharaohs’

Related

Michezo 6468171065111390172

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item