Airtel na VETA yaitambulisha VSOMO kwa makundi ya vijana jijini Arusha | LUKAZA BLOG

Airtel na VETA yaitambulisha VSOMO kwa makundi ya vijana jijini Arusha

Airtel kwa kushirikiana na VETA mwishoni mwa wiki imewafikia vijana mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, madereva wa bodaboda katika mkoa w...

Airtel kwa kushirikiana na VETA mwishoni mwa wiki imewafikia vijana mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, madereva wa bodaboda katika mkoa wa Arusha na kuwahamasisha kujiunga na masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu za mkononi ili kukabiliana na tatizo la ujuzi linalosababisha wengi kukosa ajira

Masomo hayo kwa njia ya mtandao ya VSOMO yatawapatia vijana mwanya wa kuongeza ujuzi ambapo kwa sasa kozi 5 zinapatikana hivyo mteja wa Airtel ataweza kuchagua masomo anayotaka kusoma na kisha kupatiwa vyeti vinavyotambulika katika soko la ajira.

Baadhi ya wajasiriamali na madereva bodaboda wa kituo cha MOUNT MERU jijini ARUSHA, wamesema hatua hiyo ni nzuri kwani itawapa fursa yakujiendeleza.

Akiambatana na Airtel pamoja na VETA, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Mushashu Anaclet aliongelea mpango huu na kusema” hatua hiyo itatoa fursa kwa watu wengi kupata elimu kwa muda muafa ambayo itakuwa nguzo katika maisha yao ya kila siku. Tunawapongeza Airtel na VETA kwa kuanzia mpango huu ambao utachochea kuwa na jamii wenye ueledi, ujuzi na elimu ya kutosha na kuchochea kukua kwa uchumi.

Meneja wa mradi huo, toka VETA, Mhandisi Lucius Lutenganya amesema mpango huo utaongeza wigo mpana kwa vijana wengi kuweza kusoma kwani tumekuwa tukipokea maombi maeneo mengi kila mwaka
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Mushashu Anaclet (wa pili kushoto) akiongea wakati wa kutambulisha mpango wa mafunzo ya VSOMO kwa kiongozi wa Bodaboda Kelvin Adam kuashiria uzinduzi wa masomo ya ufundi kwanjia ya simu za mkononi yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na VETA.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Mushashu Anaclet (wa pili kushoto)akitambulisha mpango wa mafunzo ya VSOMO kwa kiongozi wa Bodaboda Kelvin Adam kuashiria uzinduzi wa masomo ya ufundi kwanjia ya simu za mkononi yanayotolewa na VETA kwa kushirikiana na VETA.
baadhi ya wakazi wa mkoa wa Arusha wakipokea vipeperushi vyenye maelezo ya VSOMO.
Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba akitoa maelezo ya VSOMO kwa vijana mkoa wa Arusha.
baadhi ya wateja wakijiunga na mtandao wa Airtel ili kupata mafunzo ya VETA kwa njia ya simu zao za mkonono maarufu kama VSOMO.

Related

kitaifa 5565259482187256207

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item