BUHIGWE NA UVINZA ZAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KIGOMA | LUKAZA BLOG

BUHIGWE NA UVINZA ZAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PS3 MKOANI KIGOMA

  Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa  PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo bahash...


 Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo bahasha iliyo na majina ya Wilaya mbili zitakaanzo anza utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya seklta za Umma (PS3) Mkoani Kigoma. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
 
 Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akionesha bahasha hiyo kwa washiriki. Kushoto ni Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa
PS3, Dk Conrad Mbuya na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.

Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akitangaza majina ya Halmashauri Mbili za Wilaya ambazo zitaanza katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa PS3 mkoani Kigoma. Halmashauri za Uvinza na Buhigwe zilipita.
 Washiriki wakiwepo wakuu wa Wilaya wakishangilia kwa uteuzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mkutano huo.

Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akizungumza namna utekelezaji utakavyofanyika. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.

 Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa PS3, Dk Conrad Mbuya alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu na kuiboresha.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce Muro akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi Utumishi, Kajura wakati wa mkutano huo.
 Washiriki wakiwa katika mkutano huo. 
 Mwakilishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma akiwasilisha majadiliano yao.
 Mshiriki wa mkutano akiuliza swali
 Mkurugenzi Msaidizi Utawala kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akifafanua baadhi ya vitu wakati wa mkutano huo na hasa alizungumzia umuhumi wa uboreshaji wa idara ya Masijala ya siri katika Halmashauri.
 Washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallagyo wakati akifunga mkutano huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
***************

HALMASHAURI mbili za Uvinza na Buhigwe mkoani Kigoma zimefanikiwa kuchaguliwa kuanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) awamu ya kwanza chini ya ufadhili wa Shirika la Maemdeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
Halmashauri hizo zimechaguliwa miongoni mwa halamashauri nane za mkoa huo ambazo zipo katika mpango wa utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika mikoa 13 na utazinufaisha halmashauri 93 hadi kukamilika kwake.


Mradi huo wa PS3 ulizinduliwa mkoani Kigoma juzi na kufanya jumla ya mikoa 11 kati ya 13 iwe imeshazindua mradi huo ambapo mikoa mingine ambayo inatarajiwa kuzindua Jumanne ijayo ni Kagera na Rukwa na kufanya halmashauri 22 kati ya 93 kuanza utekelezaji wa mradi kwa awamu ya kwanza na utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kwa gharama ya dola za kimarekani Milioni 62.


Mradi huo wa PS3 utatekelezwa kwa 
awamu mbili mkoani Kigoma ambapo awamu ya kwanza inaanza mwezi huu na awamu ya 
pili itaanza Novemba mwaka huu.Awamu ya kwanza ya mradi 
itatekelezwa katika  Halmashauri  mbili zenye uhitaji zaidi katika sekta za umma
.

Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa 
PS3, Dk Conrad Mbuya alisema alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake 
na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu
na kuiboresha.Dk Mbuya alisema kwa mkoa wa Kigoma 
Halamsahauri ambazo zitaanza kunufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Wilaya Uvinza 
na Buhigwe ambazo watendaji kutoka halamshauri husika wanaanza mafunzo leo ya
siku moja na wiki ijayo madiwani wao nao watapatiwa mafunzo maaluma ya namna ya 
kushiriki katika utekelezaji wa mradi na yatafayika kwa wiki moja mjini Kigoma.


Mradi huo wa PS3 unalenga kuunda 
ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za 
umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa 
taarifa na tafiti tendaji   


Ushirkiano huo wa PS3 katika ngazi 
ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia 
ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii 
ambazo hazijanufaika vya kutosha.


Aidha Katibu Tawala wa Mkoa wa 
Kigoma, Charles Pallangyo aliwataka watendaji katika halmashauri hizo kuufanya 
mradi huo kuwa endelevu na haitakuwa busara wahisani wakiondoka na kila kitu 
kinakufa.


“Tukahakikishe kuwa mradi huu 
unakuwa endelevu na hata wahisani wakimaliza muda wao sisi tuweze kuendelea kwa
mafanikio ambayo yatazisaidia halmashauri zetu katika utendaji,”alisema 
Pallangyo.


Awamu ya pili ambayo itatekelezwa 
mkoani Kigoma   kwa halamashauri sita zilizobaki utafanyika kuanzia 
mwezi Novemba mwaka huu na utahusisha Halmashauri za Wilaya  ya Kakonko, Halmashauri ya Mji wa Kasulu,
Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Halmashauri 
ya Wilaya ya Kigoma na Halamashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao 
umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa 
na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa,
ambayo ni Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi 
ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo 
cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania 
(TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.


Mradi wa PS3 utatekelezwa katika miakoa 
13 ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, 
Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

Related

kitaifa 4542333618888145289

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item