Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya | LUKAZA BLOG

Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya

Image caption Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania Bodi ya Utalii Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya sh...

Tanzania
Image captionMlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania
Bodi ya Utalii Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.
Shirika hilo lilikuwa likiripoti kuhusu kifo cha Guguleth Zulu, raia wa Afrika Kusini, aliyefariki akikwea Mlima Kilimanjaro.
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ilisema.
Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.

Related

Hot Stories 356317531304200848

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item