NAIBU WAZIRI WA ARDHI , NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UENDELEZAJI MILIKI | LUKAZA BLOG

NAIBU WAZIRI WA ARDHI , NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UENDELEZAJI MILIKI

 Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akifungua mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki uliofa...

 Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula akifungua mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini Dar es salaam kwa lengo la kuanzisha Chama chao kwa ajili ya kusimamia masula mbalimbali ya Uendelezaji wa Miliki , Moja ya mambo yaliyojadiliwa katika mkuta no huo ni Katiba Pendekezwa ya Chama hicho ambapo wajumbe wamepata muda wa kuchangia mawazo yao na kurekebisha baadhi ya vifungu ili kuipitisha mara baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk
Angelina Mabula akizungumzia masuala mbalimbali katika  mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki  uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini  Dar es salaam
 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk  Angelina Mabula ili  akifungua mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu na Miliki Hamad Abdallah Mkurugenzi wa wakifuatilia kwa karibu wakati mkutano huo ukiendelea
 Baadhi ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia kwa karibu masuala kadhaa ambayo yamezungumziwa katika mkutano huo
 Mmoja wa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo Bw. Emilian Rwejuna akiwa pamoja na wadau wengine.
 Mkurugenzi wa Milki Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Hamad Abdallah akifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwanasheria wa Shirika hilo Elias Mwashiuya hayupo pichani wakati akitoa mada kuhusu katiba ya chama hicho  katika mkutano huo
 Itandula Gambalagi Mkuu wa Mauzo NHC akisalimiana na Bw. Adam Jee ambaye pia alihudhuria katika mkutano huo kama mmoja wa wadau wa Uendelezaji Milki.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu wakifuatilia maelezo ya Mwanasheria wa NHC Bw.Elias Mwashiuya wakati alipokuwa akielezea vifungu mbalimbali kuhusu katiba ya chama hicho.
 Mwanasheria wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC akitoa maelezo kwa wadau wa Uendelezaji Milki kuhusu Katiba ya Chama hicho ambayo wadau wamepata fursa ya kuchangia mawazo yao kabla ya kupitishwa na chama hicho
 Wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi, Hamad Abdallah Mkurugenzi wa Milki NHC, Suzan Omari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NHC na Mkuu wa Mauzo NHC Bw. Itandula Gambalagi wakiwa katika mkutano huo.

Related

kitaifa 6693996307783160466

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item