RAIS MAGUFULI AONGOZA WAKAZI WA DODOMA NA VITONGOJI VYAKE KUWAKUMBUKA MASHUJAA WA TAIFA | LUKAZA BLOG

RAIS MAGUFULI AONGOZA WAKAZI WA DODOMA NA VITONGOJI VYAKE KUWAKUMBUKA MASHUJAA WA TAIFA

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima mbeleyamnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa t...

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima mbeleyamnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa taifa mjini Dodoma Julai 25, 2016 mara baada ya kuweka Sime na ngaokwenye mnara huo ikiwa ni ishara ya kukumbuka ushujaa wao. (PICHA NA IKULU)
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho hayo.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe, Dkt.John Pombe Magufuli akiweka Mkuki na Ngao katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mashujaa katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma leo Julai 25, 2016. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)
 Wanajeshi wa JWTZ wakiwa kwenye maadhimisho hayo
NA IMMACULATE MAKILIKA- DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kudumisha amani iliyopo ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa mbalimbali kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.

Akizungumza leo, wakati akihutubia wananchi mara baada ya kumaliza shughuli za maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa  iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
Rais Magufuli alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa  ni muhimu kwa vile watu hao walijotoa kwa ajili ya kulitetea taifa.
“Wakati tunawakumbuka waliotangulia mbele za haki, sisi tuliobaki tudumishe amani hii, kama ambavyo wao waliotutangulia hawakujali dini zao bali taifa hili” alisema Rais Magufuli.

Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania imebaki kuwa kisiwa cha amani, na amani hiyo isichezwe  bali ijengwe na kudumishwa kwa umoja na mshikimamano ili kusaidia kuitangaza nchi zaidi.

Aidha, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Ali Mohamedi Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malecela nao wapewa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Viongozi hao, wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani iliyopo na kusema kuwa ni jukumu la wananchi  wote kuhakikisha  hawashiriki katika vitendo vitakavyosababisha   uvunjifu wa amani.

Ambapo, waliwataka wananchi kuwaombea Mashujaa wote waliofariki katika vita mbalimbali wakiwa  katika  harakati za kulifanya Taifa la Tanzania kuwa huru.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, alisema kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa agizo la Rais la kuitaka Serikali kuhamia mjini Dodoma.

“Nahamia Dodoma mwezi wa tisa,na nitakapohamia mawaziri wote lazima wanifuate. Katika hili nitasimamia kwa nguvu zote” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Awali, Mheshimiwa Rais Magufuli alisema kuwa atahakikisha katika kipindi cha utawala wake, Serikali inahamia mjini Dodoma, kwa vile Rais wa Awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere alionesha nia ya kufanya hivyo.

 Aliongeza  kuwa  kwa sasa mji wa Dodoma unaweza kukidhi mahitaji hayo ya Serikali kwa kutumia  miundombinu iliyopo, hata hivyo Serikali inaendelea kujenga miundombinu mipya.

Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa hufanyika Julai 25, ya kila mwaka, kwa   kufanya  maombolezo ya Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali katika harakati za kutetea uhuru wa nchi ya Tanzania.
 Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma, ambapo Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maadhimisho hayo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan
Mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliopoteza uhai wao wakilipigania taifa. Mnara huu ukomjini Dodoma ambapo leo Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Pombe Magufuli, leo Julai 25, 2016 aliwaongoza Wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake, kuwakumbuka mashujaa hao.
Rais John Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.  Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubei Ali Maulid na wapili kulia ni Spika wa Bunge, Dkt, Tulia Ackson. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016
 Waziri Mkuu Majaliwa akisalimiana na mtangulizi wake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda
 Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
 Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, 9IGP), Ernest Mangu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma, Julai 25, 2016. Majaliwa amewaahidi wananchiwa Dodoma kuwa Septemba mwaka huu, atahamia na kufanya shughuli zake mjini humo.
Wananchi wa Dodoma waliojitokeza kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma wakimsikilza Rais John Maguguli wakati alipozungumza kwenye maadhimisho hayo mjini julai 25, 2016
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maadhimisho ya uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wakishudia uwashwaji mwenge katika viwanja vya Mnara wa mashujaa Mjini Dodoma  uliowashwa na  Mkuu wa Wilaya Dodoma Mhe, Christina Solomon Mndeme

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Related

Hot Stories 5353192900771220721

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item