Ureno Bingwa Wa Ulaya baada ya kuiadhibu Ufaransa katika fainali | LUKAZA BLOG

Ureno Bingwa Wa Ulaya baada ya kuiadhibu Ufaransa katika fainali

Ilikuwa ni fainali mbovu kumalizia michuano mikali ya Euro 2016. Yaani Ureno, ambayo imenyakua ubingwa huo kwa goli moja la mshambuliaj...

Ilikuwa ni fainali mbovu kumalizia michuano mikali ya Euro 2016. Yaani Ureno, ambayo imenyakua ubingwa huo kwa goli moja la mshambuliaji wa zamani wa Swansea ya Uingereza Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes, timu iliyomaliza ya tatu kwenye hatua za makundi wamenyakua kombe wakiwa wameshinda mchezommoja tu kati ya saba ndani ya dakika 90. Hata hivyo Ureno inastahili sifa, kwanipamoja na kumpoteza nahodha wao na mchezaji Bora Cristiano Ronaldo alipoumia goti katika kipindi cha kwanza kwa kuchezewa vibaya na Dimitri Payet wa West Ham.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ureno wakishangia kwa pamoja ushindi walioupata kupitia kwa Mshambuliaji, Ederzito ‘Eder’ Antonio Macedo Lopes (9) wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji wa Mashindano hayo, Ufaransa, uliochekwa katika uwanja wa Stade de France.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Christiano Ronald pamoja na Mkongwe Ricardo Quaresma wakiwa na mwali wao mara baada ya kutwaa kwa kuwagaragaza wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016) katika mchezo uliopigwa katika dimba la Stade de France, nchini Ufaransa.
Huzuni baada ya kufungwa.

Related

Michezo 2608337300200964587

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item